LivingIslam.org presents:

Mapishi - RECEPIES ZA KIZANZIBARI

1.VILOSA
2.MEAT CAKE
3.EGG SANDWICH
4.SWISS ROLL
5.JAM BUNS
6.TRAFIC LIGHT BISCUITS
7.DINNER ROLL
8.COCONUT BUNS
9.BUTTER ICING
10.CHOCOLATE CAKE
11.RAISSING CAKE
12.SAMAKI WA KUKAANGA
13.SCHOO YA NYAMA
14.MEAT CURRY
15.BANANA & MEAT STEW
16.FISH ROLLS
17.PAI YA SAMAKI
18.PAI YA NYAMA
19.LEMON PUDING
20.LEMON BISCUITS
21.MKATE WA NDIZI MBIVU
22.VILEJA VYA NJUGU
23.VIKAAKAA
24.SAMBUSA ZA KUOKWA
25.VICTORIA SANDWICH
26.MKATE WA TANGAWIZI
27.SALADI YA MATUNDA
28.KARI YA SAMAKI
29.KITAWA
30.VIKONI
31.COCONUT PRAYMIDS
32.FARNE
33.PINUT BUTTER
34.VIDUDE
35.FAGI
36.TOFI
37.HALF CAKE
38.PERA MAZIWA
39.NANGATAI
40.VILEJA VYA CHUMVI
41.BISKUTS
42.MKATE WA KUUKAANGA
43.MKATE WA MAYAI NA JAM
44.MKATE WA NYAMA (MSANIF)
45.MKATE WA NYAMA MTABAK
46.MCHUZI WA NYAMA NA DENGU
47.MKATE WA KIAJEMI
48.KUKU WA KUJAZA
49.BOKOBOKO
50.MCHUZI WA BOKOBOKO
51.KASHATA ZA MAYAI
52.KASHATA ZA NJUGU
53.KABABU ZA NYAMA
54.UJI WA MAZIWA NA ZABIBU
55.FALUDA
56.FARNE
57.BIRIANI YA SAMAKI
58.NYAMA YA KUIKIZA
59.TAMBI ZA KUKAANGA
60.VILEJA
61.KUKU WA KUCHOMA
62.KUKU WA KUPAKA
63.MCHUZI WA KABABU
64.SAMAKI WA MAYAI
65.WALI WA ASUMINI
66.WALI WA BIRIANI
67.MKATE WA CHILA
68.MKATE WA KUMIMINA
69.MKATE WA MAYAI
70.VIKATE VYA ZAFARANI
71.VIKATE VYA JOYA
72.MCHUZI WA KIMA
73.MCHUZI WA M AINI
74.SAMBUSA ZA MAFUTA
75.KATLES ZA SAMAKI
76.SAMBUSA ZA BWANA
77.KACHORI
78.VITUMBUA
79.SAMAKI WAKUPAKA
80.SAMAKI WA ROJO
81.WALI WA PILAU
82.WALI WA CHOOKO
83.MAANDAZI YA KIPEMBA
84.MKATE WA CHANDARUA
85.MKATE WA UFUTA
86.MKATE WA KIAJEMI WA KUKU
87.FILLING
88.POTATO PIE
89.MOUSAKA
90.MEAT CAKE
91.COCONUT &GROUND N.Q. CAKE
92.VIKAIMATI
93.NANGATAI
94.GROUND NUT BISCUITS
95.MEAT BISCUITS
96.BISCUITS ZA MAYAI
97.KASHATA ZA NJUGU ZA KUSAGA
98.MKATE WA TAMBI
99.CHALLAH BREAD
100.BOKOBOKO YA NGANO
101.MKATE WA MCHELE
102.BASHAMELL (MAKARONI)
103.CHOCOLATE MOOSE
104.ICE CREAM YA LOZI
105.SUPER GET YA KUKU
106.MCHUZI WA ADESI
107.FISH FINGER
108.BUTTER BOLLS
109.PUDDING
110.PIZZA – MEAT
111.VILILI
112.TUTTY FRUITS
113.KARA BISCUITS
114.BISCUITS ZA TANGAWIZI
115.ROCK CAKE
116.ROCK BUNS
117.ALMOND SLICES
118.DOUGHNUTS (DONAS)
119.PUDDING YA POVU
120.LADU
121.BISCUITS ZA VIDOLE
122.QUEEN'S CAKE
123.KEKI YA JABALI
124.COCONUT BUNS
125.MELTING MOMENTS.



VILOSA

Semolina * cup

Rice 1cup

Eggs 3

Nido kikombe cha kahawa1

Sukari 2 cups

zafarani kiasi

Rose arki kiasi

Method:

Roweka mchele ukisha rowana uchuje mpaka utoke maji yote tia kwenye
blander pamoja na mayai, zafarani, arki (maziwa unatia kwenye kikombe cha
unakoroga) ndio unatia pamoja, baadae unatia na hamira saga pamoja kidogo
uchanganyike baadae tia semolina usage tena sana mpaka iwe laini kama
vitumbua ikisha utatia nido kikombe 1 cha kahawa na sukari utakisia,
baadae saga tena uchanganyike uwache uumke na uchome kama vitumbua
lakini hivi unatia shira mwisho.

SHIRA

Sukari 2tea cup, Maji 21/2cup, zafarani + rose essense

Method: fanya shira kama ya kaimati (iwe inanata)



MEAT CAKE

Nyama 11/2kg (ya kusaga)

Siagi 1/4kg

Unga1/4kg

Carrot1/4kg

Pilipili mbuzi 1/4kg

Mayai 18

Uzile

Mdalasini

Pili pili manga

B.powder 2tsp

Ndimu 1

Thomu kidogo

Method:

Changanya nyama, thomu, ndimu, pilipili manga, mdalasini na uzile na upike
pamoja iwive kasha saga siagi na mayai 6 hadi iwe cream na nyepesi kama
unavyofanya kwa keki ya sukari kasha changanya pamoja kwa unga na
B.powder changanya kwa mkono mpaka uchanganyike piga mayai mengine 6
na uchanganye na ile nyama kwa kijiko mpaka ichanganyike vizuri. Para
carrot zako kwa kutumia kile kibati cha kuparia chips nazo ziwe kama chips
tena zichemshe kidogo ziwive, kata pilipili boga ziwe slices za duara
nyembamba. Mwisho paka trey yako siagi itandaze ienee yote na mimina ule
mchanganyiko wa cake juu yake halafu tandaza juu yake ule mchanganyiko
wa nyama na mayai, tena vunja mayai 6 yalibakia uyapige vizuri, tandaza
carrots zako juu yake na zile slices za pili pili boga, kasha malizia kwa
kunyunyiza mote yale mayai uliyoyapiga tia ktk oven pre-heated temp. 180C
mpaka ikauke na iwive na ikipoa kata square na uwandae.

SANGWEJI YA YAI (Egg Sandwich)

Yai moja lililochemshwa

Siagi * oz

Pilipili ya unga kiasi

Nyanya 1 (tungule)

Vipande 6 vya mkate (vilivyokatwa vipande vyembamba)


Njia:

Paka siagi kwenye vipande vya mkate

Piga yai (Siere) ndani ya bakuli. Ongeza * oz

Weka mchanganyiko wa yai ya vipande 3 vya mkate.

Menya nyanya na kata vipande vyembamba na weak nyanya juu ya
mchanganyiko wa yai.

Weka kipande kingine cha mkate kilichopakwa siagi juu ya vipande vyote
vya mkate vyenye mayai kata na ondoa sehemu ngumu ya pembeni.

Kata mkate pembe 3 na andaa kwenye sahani.



SWISS ROLL


Mayai 4

Unga wa ngano oz 4

Sukari oz 4

B.powder vijiko vya chai 2

Jam vijiko vya mezani 2

Sukari laini kijiko cha mezani 1

Ganda la limau au 1/2tsp (vanilla)

Njia:

Paka mafuta kwenye legeni

Kata karatasi isyonyonya mafuta (geese ca of paper) ukubwa wa legeni na
inchi 1 zaidi, weka karatasi hii ndani ya legeni na paka mafuta juu ya
karatasi.

Weka sukari ndani ya bakuli na mayai piga piga mchanganyiko mpaka uwe
mweupe chekecha unga kidogo kidogo juu ya mchanganyiko na koroga hadi
unga wote umeisha ongeza ganda la limau.

Mimina mchanganyiko kwenye legeni na oka katika oven yenye joto
170C./350F kwa dakika 7-10.

Epua na ondoa keki kwenye legeni ondoa karatasi haraka.

Paka jam kwenye keki kisha viringisha kufuata upana wa keki nakata
vipande vya kiasi.

Waweza kunyunyiza sukari laini juu ya jam. Andaa


JAM BUNS/ANDAZI LA JAM


Unga wa ngano 8oz

Hamira ya unga vijiko vya chai tsp2

Mayai 2

Jam vijiko vya kulia 2

Siagi vijiko vya kulia 2

Sukari vijiko vya kulia 4

Maziwa * kikombe



Njia:

Chekecha unga na hamira kwenye bakuli kubwa

Fikicha siagi na unga hadi mchanganyiko ufanane na chenga za mkete.

Ongeza sukari na changanya vyema.

Ongeza yai lililopigwa mara 2 na maziwa na changanya vyote vizuri ili kuwe
na donge laini. Washa oven 250F-300F au 140C-150C.

Tengeneza shimo katikati ya kinyunga kwa kidole na weka juu jam kidogo.

Tengeneza vimviringo vidogo vidogo kwa kiganja cha mkono.

Paka mafuta legeni na weka vile vimviringo kwenye legeni.

Oka kwenye Oven kwa muda wa dakika 15 – 20

Epua na tayarisha



TRAFIC LIGHT BISCUITS


Sukari oz 2

Siagi oz 2

Yai 1

Arki matone 4

Pinch ya chumvi

Unga wa ngano oz 4

Hamira unga kijiko cha chai 1

Jam kijiko cha kulia 2

Sukari laini

Food 1 Coularing kijani na nyekundu matone machache

Njia:

Tindia sukari na siagi pamoja hadi vichanganyike vizuri

Ongeza lawani chekecha unga,chumvi na hamira juu ya mchanganyiko ili
kufanya kinyunga. Ongeza maziwa kidogo kama ni lazima

Sukuma kinyunga hadi kiwe na unene wa * inch na kata mviringo miwili.

Paka mafuta legeni na oka biskuti ambazo hazijatobolewa kwenye oven
yenye joto 150C hadi iive.

Kata biscuits zilizobaki ili ziwena mashimo 3 kila kwenye biscuit kisha oka.
Ongeza matone machache ya rangi nyekundu ya chakula kwenye oven kwa
muda wa dakika 15-20.


DINNER ROLLS

Unga wa ngano 8oz

Sukari tsp 1

Siagi 1oz

Chumvi tsp1

Hamira tsp 1

Maziwa ya uvugu uvugu kikombe 1

Yai 1

Njia:

Chekecha unga na chumvi kwenye bakuli kubwa

Fikicha siagi na unga

Tengeneza shimo katikati ya unga na tia sukari na hamira. Changanya ili
kufanya uji mwepesi sana. Funika na weka mahali pa uvugu uvugu kwa muda
wa dakika 10-15.

Hamira ikisha umuka changanya unga na maziwa au maji ya uvugu na fanya
kinyunga kanda kiunga vizuri na bila kuongeza unga ikiwezekana.

Acha kinyunga kiumuke mara mbili ya ukubwa wake kisha kanda tena.

Tengeneza maumbo mbali mbali kisha acha ili uumuke tena weka kwenye
legeni.

Piga piga yai kisha paka juu ya rolls oka kwenye oven yenye joto 300F –
350F au 170C – 180C kwa muda wa dakika 15-20 epua.



COCONUT BUN


Unga wa ngano oz 4

Hamira ya unga kijiko cha chai 1

Machicha ya nazi (yasiochujwa) oz 1

Siagi oz 2

Maziwa kijiko cha kulia 1*

Siagi oz 2

Yai 1 pich ya chumvi.

Njia:

Chekecha unga hamira na chumvi kwenye bakuli ongeza siagi fikicha
mchanganyiko vema. Ongeza sukari na nazi changanya vizuri. Pasua yai
lipigepige na ongeza kwenye mchanganyiko pamoja na maziwa hadi
mchanganyiko ushikamane vizuri.wika mchagayiko kwenye legeni yenye
shimo uliyoipaka mafuta na oka kwenye oven yenye joto 200ckwa
dakika20.Epua na andaa.


BUTTER ICING

Siagi 2

Maziwa kijiko kikubwa 1-2

Sukari laini oz 6

vanila tone 3



Njia:

Tindia sukari na siagi hadi iwe laini sana

Ongeza lawani na changanya vema

Tayari.

N.B waweza kuongeza maziwa kidogo. Huweza kutumika kwa

kupaka juu au hujaza kuremba keki


CHOCOLATE CAKE

Siagi oz 6

Mayai 3

Vanilla kijiko cha chai1

Pinch ya chumvi

Unga oz.7.

Cocoa oz.1

Hamira unga kijiko cha chai

Maziwa fresha kidogo

NJIA

1. Tindia sukari na siagi hadi iwe nyepesi

2. Ongeza yai lilopigwa kidogo na koroga kila baada ya kuongeza
mayai.

3. Chekecha unga, cocoa,hamira na chumvi, juu ya mchanganyiko wa
mayai. Ongeza vanilla na maziwa kidogo ili kupata mchanganyiko laini
kiasi.

4. Paka mafuta kwenye legeni weka karatasi na kuipaka mafuta na waha
oven170C-180C.

5. Weka mchanganyiko kwenye legeni na oka kwa muda wa saa 1.
ikipowa andaa.pamba kwa sukari laini chekecha juu yake.



RAISSING CAKE (KEKI YA ZABIBU)



Siagi kikombe *

Sukari kikombe1

Mayai 3

Unga wa ngano vikombe2

Hamira tsp 1

Chumvi tsp 1

Maziwa fresh *

Cocoa *.

Njia

Paka siagi kwenye legeni ya keki na nyunyiza unga kidogo.pasha maji moto
na weka zabibu ndani ya maji ya moto na kuzitoa mara moja.Zichuje maji na
kuzikausha kwa kitambaa safi cheupe. Tindia sukari na siagi hadi iwe laini
na nyeupe wv aha oven joto 170c-180c. pigapiga mayai na kuongeza
kidogokidogo kwenye mchanganyiko.ongeza chavi chakecha hamira na unga
juu ya mchanganyiko na koroga kwa ongeza zabibu kama mchangayiko ni
mzito sana ongeza maziwa kidogo.Mimina mchangayiko kwenye legeni na
sawazisha juu. Oka kwenye oven kwa muda wa dakika 35-45.

N.B unaweza kupamba keki hii kwa butter icing.


SAMAKI WA KUKAANGA(SHALLOW FOR FRYING


Minofu 2 ya samaki mbichi

Yai 1 piga

Chumvi kiasi

Mafuta

Maji tbl sp 2

Chenga za mkate tb. Sp 2

Njia

1. Osha minofu ya samki ikaushe maji na ipake chumvi na pilipili.

2. Weka vipande vya samaki kwenye yai na vibinginishe kwenye
chenga za mkate.

3. Kanga minofu ya samaki hadi iive na ibadilike rangi ya kahawia.epua
andaa
SCHOO YA NYAMA (BROW STEW)



Nyama nusu kilo

Vitunguu viwili

Karot 2

Nyanya 2

Unga wa ngano oz2

Pilipili hoho1

Bizari tsp1

Chumvi tsp1*

Mafuta maji vijiko vya mezani 2

Vitunguu thomo vidole 4

Viazi mviringo2

Pilpili ya ung oz *

Njia

1. Katakata nyama na chemsha maji kidogo na chumvi.

2. Menya na katakata vitunguu vipande vidogovidogo sana.

3.Menya nyanya, na katakata, menya viazi na vikate vipande 4

kila kiazi.

4. Menya na katakata karoti kwa marefu na pilipili hoho. Menya na
vitunguu thomu viponde.

5. Pasha mafuta moto na kanga unga wa ngano mpaka uwe rangi ya
kahawia.

6. Paka mafuta yaliyobaki na kaanga vitunguu maji na thomu, kisha
ongeza nyama (b mchuzi)

7. Ongeza nyanya,karot, pilpili hoho na viazi,chumvi na bizari kisha
koroga vyema.

8. Tengeneza rojo zito kwa kutumia unga uliokaangwa na maji kidogo
ya uvuguvugu kisha mimina rojo katika nyama na koroga vyema

9. ongeza mchuzi wa nyama na maji kidogo iwapo ni lazima.

Acha school iendelee kutokota taratibu mpaka viungo vyote viive vyema.
Epua na andaa pamoja na chakula chochote.


MEAT CURRY


Nyama oz 8

Bizari oz 1

Vitunguu 3 vilivyolengwa

Pilipili 1

Thomu tembe 2

Tangawizi iliyosagwa

Mafuta ya maji oz 2

Nazi1

Limau1/4.

Njia

1. Safisha nyama na kata vipande vidogovidogo.

2. Ongeza kitunguu thomu, thangawizi na bazari kwenye nyama
changanya vizuri iwache kwa muda viungo vikolee.

3. Kamua na chuja tui la nazi mara tatu.

4. Pasha moto mafuta na kanga vitunguu hadi viwive, Ongeza vitunguu
na nyanya na endelea kukaanga kwa dakika2

5. Ongeza tui la nazi ulilokamua mara ya pili na tatu changanya vizuri
na koroga na acha ichemke.Ongeza tui la kwanza,punguza moto na
kuacha nyama iendelee kutokota.

6. Epua na ongeza kijiko kidogo cha maji ya limau koroga vuzuri na
andaa.

Kari ya nyama yaweza kuandaliwa na wali au mkate.

BANANA & MEAT STEW

Nyama steki oz 4

Ndizi mbichi 4

Nazi1/2

Nyanya

Kitunguu maji na thomu 1

Mafuta ya maji tsp1

Chumvi

Pilipili unga 1/2tsp.

Njia

1. Osha nyama na ikate kate kisha itokote hadi iwive kiasi.

2. Menya na katakata ndizi zioshe na kuziweka kwenye chombo cheye
maji baridi.

3. Tayarisha tui la nazi kikombe kimoja.

4. Menya na katakata vutunguu, menya nyanya na katakata.

5. Pasha mafuta moto kisha kanga vutunguu ongeza nyanya, nyama,
ndizi na tui la nazi.

6. Tokosa chakula hadi ndizi ziwive.


FISH ROLLS


Samaki 2 wabichi waliochemshwa

Viazi mviringo vilivyochemshwa na kupondwa

Siagi tsp 1

Yai lililopigwa

Chenga za mkate

Maziwa fresha 2tsp

Chumvi 1 tsp

Chumvi 1tsp

Pilipili ya unga

Njia:


Ondoa ngozi na mifupa kwenye samaki na chambua minofu. Ongeza viazi
vilivyopondwa na siagi, ongeza pili pili na chumvi, ongeza nusu ya yai na
changanya vizuri kama mchanganyiko ni mkavu ongeza maziwa, changanya
vyema na tengeneza mviringo mirefu 4, pakaza yai lililobakia na viringisha
samaki (rolls) kwenye chenga za mkate. Paka legeni mafuta na kuoka rolls
kwenye oven na joto 170 – 180 degrees F. kwa muda wa dakika 20 – 25.
andaa pamoja na tomato sauce.

N.B waweza kukaanga rolls kwenye mafuta (kwa kutosa) hadi iwe rangi
kahawia na hudhurungi baada ya kuokwa.


PAI YA SAMAKI

Samaki oz 12 (minofu iliyochemshwa)

Viazi vidogo 3 vilivyochemshwa

Nyanya ndogo 3

Macaroni oz 2, (yaliyochemshwa na kupakwa siagi, chumvi, Jimbini 2 oz

Pilipili ya ungaa * tsp

Siagi oz 1

Mayai 2

Maji yaliyochemshiwa samaki * kikombe

Chenga za mkate oz 1.

Njia:

Paka mafuta kidogo, piga piga mayai ndani ya bakuli na ongeza minofu ya
samaki yalichambuliwa na nusu ya viazi vilivyopondwa, chumvi, pilipili na
macaroni, ongeza mchuzi wa samaki na changanya vizuri. Pakua nusu ya
mchanganyiko ndani ya pie dish. Panga nyanya zilizokatwa slice za * ikisha
ongeza mchanganyiko uliobaki na panga tena nyanya zilizobaki. Funika na
mchanganyiko wa viazi vilivyobaki.

Nyunyiza jibini na chenga za mkate juu ya pie kisha paka (dondosha) siagi
kidogo kidogo juu yake. Oka katika oven yenye joto 125-150 deg.C. mpaka
pie iwive na iwe rangi ya kahawia epua.

PAI YA NYAMA


Nyama ya kusaga oz 6

Karoti 1

Kitunguu 1

Nyanya 1

Giligilani 2tsp

Chumvi 1 tsp

Yai lililopigwa

Maziwa 2oz

Siagi 2tsp

Viazi mviringo vilivyopikwa na kupondwa 6oz.

Njia:

Pika nyama hadi iwive, Menya kitunguu na karoti na kata vipande vidogo
vidogo. Menya nyanya na katakata, pasha mafuta moto na kanga viungo
vyote, ongeza nyama na maji kidogo visiwe vikavu sana, Ponda viazi vingali
moto ongeza siagi, maziwa na chumvi, Paka mafuta chombo cha kuwekea
pai (pai dish) na weka mchanganyiko wa nyama ndani. Tandaza viazi juu ya
nyama. Sawazisha kwa kisu. Tengeneza viumbo lolote juu ili kupamba. Paka
yai juu ya viazi kisha oka kwenye oven yenye joto 160deg C. hadi pai iwe
kahawia. Epua na andaa pamoja na mchuzi rojo. N.B. unaweza kupaka
maziwa juu badala ya yai.


LEMON PUDING



Siagi 2oz

Sukari 3oz

Yai lililopigwa

Unga wa ngano 4oz

BP. kijiko cha chai 1

Limau 1

Maziwa kidogo.

Njia:

Saga sukari na siagi hadi vilainike vizuri. Ongeza yai kidogo kidogo na
ongeza ganda la limau.(grated lemon rind) changanya vyema. Chunga unga
na hamira juu ya mchanganyiko kwa kukoroga. Ongeza maji na limau na
koroga vizuri. Ongeza maziwa kidogo ili kupata mchanganyiko lakini,
chemsha maji, mimina mchanganyiko kwenye bakuli lililopakwa mafuta na
funga bakuli kwa foil paper pika kwa mvuke kwa nusu saa. Epua na andaa
pamoja na custurd sauce.

LEMON BISCUITS


Unga wa ngano 4oz

Siagi 2oz

Kiini cha yai 1

Sukari 2oz

Ganda la limiau lililokunwa.

Njia:

Paka legeni mafuta, chekecha unga na fikicha siagi hadi mchanganyiko
ufanane na chenga za mkate. Ongeza sukari na ganda la limau. Ongeza kiini
cha yai lililopigwa, ongeza na maji baridi kidogo hadi kiwe laini na kufaa
kusukumwa, sukuma kinyunga hadi kiwe na unene wa 3 kata mviringo ya
biscuits na weka kwenye legeni. Toboa mashimo ya urembo oka biskuti
kwenye oven zikiwiva epua na nyunyiza sukari ukipenda.

MKATE WA NDIZI MBIVU


Unga wa ngano vikombe 2

Skari kikombe 1

Siagi kikombe 1

B.powder 1tsp

Ndizi mbivu 4

Maziwa fresh kikombe 1

Mayai 2

Chumvi.

Njia:

Saga sukari na siagi hadi iwe laini na nyeupe. Menya ndizi na ziponde hadi
zilainike vizuri, piga piga mayai na kuongeza maziwa. Chekecha unga,
hamira na chumvi pamoja kwenye bakuli kubwa. Ongeza maji kidogo kidogo.
Ongeza ndizi kwenye unga na koroga ili vichanganyike vyema. Paka mafuta
kwenye legeni ya mkate na nyunyiza unga kidogo. Weka mchanganyiko
kwenye legeni na oka mkate kwenye oven joto 180deg C. kwa muda wa saa
1-1* epua na andaa.

VILEJA VYA NJUGU


Unga kibaba 1*

Siagi *

Sukari kikombe kimoja

Arki

Hiliki

B.powder

Njugu kikombe

Mayai 4.

Njia:

Saga siagi na sukari mpaka iwe laini sana. Ongeza unga, b.p, na arki
chganganya vizuri. Piga mayai na nyunyiza njugu kidogo kidogo kwenye
mchanganyiko. Kata madonge mawili, moja dogo moja kubwa, donge dogo
changanya njugu, sukuma donge la unga wa ngano kwanza halafu weka
jengine la njugu kati sukuma halafu weka tena donge la unga wa ngano
sukuma. Weka vyote kwa pamoja kata design.


VIKAAKAA

Unga wa ngano 1* kg

Siagi *

Samli *

Sukari ya kusaga *

Hiliki

Arki

Hamira 2tsp

B.powder 1tsp.

Njia:

Tia unga, hamira, siagi bp, na iliki, fikicha mchanganyiko. Chemsha samli
iwache ipoe na mimina kwenye unga kwa kunyunyizia kidogo kidogo, tia arki
uchanganye kidogo ili unga ushikane, kata madonge makubwa makubwa na
weka kwenye kibao na sukuma na kata design. Oka kwenye oven viwache
view rangi ya cream visiwe rangi ya brown na nyunyiza sukari kabla
havijapoa.

SAMBUSA ZA KUOKWA

Unga wa ngano 8oz

Siagi 4oz

Yai 1 lililopigwa

Chumvi

Viazi mviringo vilivyokatwa vipande vipande

Maji baridi ya kuchanganya

Karoti 1

Nyama ya kusaga.

Njia:

Chekecha unga na chumvi pamoja kisha fikicha unga na chumvi pamoja hadi
mchanganyiko ufanane na chenga za mkate.

Ongeza maji kidogo kidogo na changanya kwa kutumia kisu fungutu hadi
mchanganyiko usukumike. Kanda kinyunga kisha viringa kwenye jalibosi
(foil paper) na weka kwenye friji kwa muda wa dakika 15, paka mafuta legeni
ya kuoka, pika nyama hadi iwive. Sukuma nusu ya nyunga kwa urefu hadi
kiwe na unene 1/8 menya viazi na karoti na kata kata vipande vidogo vidogo
pika hadi ziwive, changanya na nyama. Weka sehemu nusu ya nyama
katikati ya kinyunga na paka maji baridi kwenye upande mmoja wa kinyunga
na pembeni unganisha pande 2 za kinyunga na paka maji baridi kwenye
upande mmoja wa kinyunga na pembeni unganisha pande 2 za kinyunga na
shikamanisha sehemu iliyopakwa maji, kata vinyunga vyenye urefu wa 2* na
weka kwenye legeni paka yai juu y akinyunga. Kata sehemu ya juu ya
kinyunga kata sehemu ya juu ili kupata nafasi ya kutoa mvuke na oka.

Sukuma kinyunga cha pili na kata mviringo mkubwa kiasi. Weka nyama
katikati na paka maji upande mmoja kisha unganisha kinyunga.

Weka urembo pembeni kwa kutumia unga. Tomoa matobo 3 juu ili kupata
nafasi ya kutoka mvuke. Weka kwenye legeni ya kuokea. Paka kinyunga yai
lililopigwa na oka kwenye oven.



VICTORIA SANDWICH

Unga wa ngano 6oz

Mayai 4

Jam vijiko vya mezani 2

Siagi 4oz

Chumvi mziwa kidogo.

Njia:

Saga mchanganyiko wa sukari na siagi hadi uwe laini na mwepesi kidogo,
pasua mayai na pigapiga na ongeza kwenye mchangayiko kidogo kidogo.
Chekecha unga, chumvi na changanya kwenye mchangayiko kidogo kidogo.
Ongeza maziwa hadi mchangayiko uwe mweupe kidogo (unaomiminika) Paka
mafuta legeni 2 na weka mchanganyiko wa keki kwenye legeni zote. Oka
kwa dakika 20 kwenye oven.

Keki ikiiva epua na acha ipoe. Paka jam juu ya keki moja sehemu ya chini na
shikamanisha na keki ya pili. Nyunyiza sukari laini juu au pamba
upendavyo.


MKATE WA TANGAWIZI


Unga wa ngano 8oz

Tangawizi ya unga vijiko vya chai 2

Bp 2 tsp

Chumvi * tsp

Sukari laini 4oz

Siagi 30z

Golden syrup 6 oz

Maziwa * pint

Yai1

Hamira ya soda * tsp.

Njia:

Paka mafura kwenye legeni ya kuokea mkate. Weka karatasi isiyonyonya
mafuta. Kisha paka mafuta kwenye karatasi. Chekecha unga, tangawizi
chumvi na hamira ya soda kwenye bakuli kubwa. Yeyusha sukari na siagi
kwenye sufuria na ongeza golden syrup na angalia zisipate moto sana pasua
yai lilopigwa pigwa na changanya ongeza maziwa. Ongeza shira ikiwa na
uvuguvugu kwenye unga. Kisha ongeza mayai na changanya vyote vizuri.
Mimina mchanganyiko kwenye legeni na oka vizuri kwa muda wa saa 1*
kwenye oven joto 163/177 deg.C punguza moto baada ya muda epua keki na
acha ipowe.

SALADI YA MATUNDA

Ndizi mbivu 3

Machungwa 2

Sukari 2 tsp

Limau

Parachichi

Papai *

Njia

Osha na kausha limau kisha kamua ili kupata ganda la limau.Chemasha
ganda la limau kwenye maji pamoja na sukari kwa dakika 5. Menya papai na
katakata vipande vidogovidogo kiasi vya mraba. Osha ndizi na katakata
mviringo mdogo.Nunyiza maji ya limau kwenye ndizi ili zisigeuke rangi kuwa
nyeusi.Osha na menya chungwa ondoa mbegu na ngozi kisha kata kila
kipande sehemu 2 changanya matunda yote vizuri kisha funika. Pooza shira,
chuja kiasi kisha ongeza kwenye saladi ya matunda na weka kwenye frigi ili
ipowe andaa.



KARI YA SAMAKI


Mnofu wa samaki4oz

Nyanya 1

Kitunguu maji

Thomu

Bizari

Limau

Maziwa fresh

Mafuta ya maji.

NJIA

Safisha samaki na kata vipande.Menya na katakata vitunguu,na ponda
vutunguu thomu.Osha na menya nyanya ikate vipande vidogovidogo. Pasha
moto mafuta na kaanga vitunguu. Ongeza viungo vyengine na endelea
kukaanga. Ongeza nyanya na endelea kukaanga, zikilainika ongeza samaki
na maziwa na endelea kupika taratibu kwa muda wa dakika 10-15. Ongeza
maji ya limau na endelea kutokosa kwa dakika 3 zaidi. Epua na andaa.


KITAWA
Ndizi mbichi 6

Chumvi

Maziwa ya mgando

Njia:

Menya ndizi na kata vipande vifupi. Safisha ndizi vizuri hadi utomvu utoke,
kisha zichemshe hadi zilainike vizuri, ziponde kisha zichanganye na maziwa
ya mgando hadi kuwa kama uji mzito. Pakua na andaa.



VIKONI

Unga wa ngano

Pilipili manga

Chumvi

Siagi

Nyama ya kusaga iliyochemshwa na kutiwa viungo.

NJIA

Changanya unga na samli, chumvi na pilpili manga mpaka vichanganyika na
kua kitu kimoja kata madonge na sukuma kwenye kibao.Kata kwa umbo la
duara na weka nyama yako katikaati. Pasua kidogo kwa kisu pinda duara na
ikae kama koni na nyama itokeze juu. Choma kwa oven au kwa makaa na
vikikaribia wekundu epua.


COCONUT PYRAMIDS


Nazi kuna anika

Sukari ya unga

Unga wa ngano

Ute wa mayai

Njia:

Piga ute wa mayai kidogo changanya na vitu vyote ukiona mzito tia maji
kidogo. Weka umbo la minara kidogo juu ya bati lililopakwa samli na
pambia.

FARNE


Unga wa mchele

Maziwa yaliyochemshwa

Iliki na sukari

Njia:

Teleka maziwa na yakichemka tia sukari na iliki wacha yachemke tena
kidogo. Tia unga uliovurugwa kwa maji na wacha uchemke kidogo. Ukiwiva
epua na mimina ndani ya bakuli. Wacha ipoe na kata vipande. Tayari kwa
kula.


PEANUT BUTTER


Njugu * kg

Chumvi

Siagi 2 tsp

Njia:

Kanga njugu toa maganda na zitwange ziwe unga. Tia chumvi kidogo, tia
siagi changanya, fanya madonge kiasi. Kula.


VIDUDE

Unga wa mchele

Siagi

Mayai

Sukari

Ufuta na iliki

Njia:


Chan>ganya unga na sukari na iliki zilizosagwa. Vunja yai na utie pamoja na
siagi. Kanda mpaka ushikane vizuri usiwe na madonge makavu. Kata
madonge makubwa na usukume juu ya kibao kwa kutumia kifimbo. Kata kwa
kibati chenye umbo la kashata huku unazipanga kwenye sinia iliyopakwa
samli. Vunja mayai na upake juu yake. Nyunyiza ufuta na vipambie vikiwiva
epua.


here
FAGI

Maziwa chupa 1

Sukari kilo moja

Samli au siagi * kg

Iliki



Njia:

Teleka maziwa changanya na siagi, iliki na samli. Koroga mpaka iwe nzito,
paka samli ndani ya sinia tandanza na weka miraba kata vipande vipande
tayari kwa kula.





TOFI



Maziwa ya kibati

Maji * kikombe

Hiliki

Sukari na arki kiasi



Njia:

Teleka maziwa changanya maji, sukari arki na iliki koroga usiwache mkono
mpaka iwe nzito. Tia samli kidogo na epua. Tandaza kwenye sinia
iliyopakwa samli na kata.



HALF CAKE



Unga wa ngano

Mayai

mafuta ya kuchomea

Nazi 2 au maziwa * chupa

B. powder

Hamira kidogo.





Njia:

Kanda unga utie sukari, arki, iliki, Bp na tui la nazi au maziwa. Ukande
mpaka uwe laini, usukume katika kibao na ukate kama maandazi kisha
choma ndani ya mafuta kama maandazi.



PERA MAZIWA



Maziwa chupa 1

Sukari kikombe 1

Unga * kg

Iliki na arki



Njia:

Changanya unga pamoja na sukari iliki na arki. Teleka huku unakoroga
mpaka uwe mzito usiwache mkono ukaja ukaganda ukafanya madonge.
Ukiwa ushaanza kuwa mzito mimina ndani ya sinia iliyopakwa samli iweke
duara kwa kikombe cha kahawa ikiwa tayari toa.



NANGATAI

Sukari * kg

Samli * kg

Arki au iliki

Unga kilo kasorobo



Njia:

Yayusha samli ili iwe kama mafuta ya kawaida, iwache ipoe saga sukari ili
kurahisisha uyayukaji. Changanya samli na sukari mpaka sukari ilainike, tia
mayai yaliyovunjwa na changanya vizuri chunga unga kisha changanya vizuri
chunga unga kisha changanya na b. powder na iliki changanya kwenye
mchanganyiko wa sukari na samli. Ukichanganya kata vidonge na vibamize
kwa mkono juu yake ili viweze kufanyika umbile maalum.



VILEJA VYA CHUMVI



Siagi *

Unga wa ngano 1kg

Mayai 2

Jam



Njia:

Changanya unga na siagi mpaka uchanganyike sawa sawa, kama mgumu tia
maji baridi kidogo. Kata nakshi uipendayo huku ukipaka yai na jam juu yake.
Choma na wacha vipoe.



BISKUTI



Unga wa ngano 2cups

Maziwa 1 cup

Sukari 1cup

Siagi 2tsp

B.powder



Njia:

Chunga unga na BP katika bakuli, fikicha siagi na unga kwa ncha ya vidole,
weka tobo kati kati ya unga na weka maziwa na sukuma. Kata madonge na
sukuma kwenye kibao na kata nakshi uipendayo. Choma.



MKATE WA KUKAANGA KWA MAZIWA NA MAYAI



Maziwa * painti

Samli * kg

Mayai 3

Chumvi kiasi

Pilipili manga kiasi

Boflo moja kubwa.



Njia:

1. Kata mkate wa boflo vipande kiasi. Piga mayai na chumvi kidogo na
pilipili manga.

2. Teleka chuma utie samli. Ikianza kuchemka chukua viapnde vya
mkate uvichovye mayai kisha uvitie katika chuma uvikaange. Vikiwa
vimewiva upande mmjoa geuza upande wapili vikiwa tayari vitoe na
uvitie kwenye sahani.



MKATE WA MAYAI NA JAM



Boflo mkubwa 1

Mayai 4

Unga wa ngano kidogo

Jam kidogo

Samli * kilo



Njia:

1. Kata mkate vipande vyembamba vyembamba uvipake jam. Kisha
vigandanishe kimoja juu ya kingine.

2. Vunja mayai uyapige sana. Kisha nyunyiza unga huku ukiendelea
kuyapiga mayai.

3. Teleka chuma utie samli. Ikianza kuchemka vichovye vile vipande
vya mkate ndani ya mayai na uvichome ndani ya samli.

Vikiiva upande mmoja geuza upande wa pili kisha uvitoe uvitie kwenye
sahani.



MKATE WA KIAJEMI



Unga wa ngano kilo 1

Samli kidogo

Hamira soda kiasi

Chumvi kiasi



1. Changanya unga, samli kidogo sana,hamira soda na chumvi na
ukande kwa maji, usiwe mgumu wala laini sana Kisha uache uumuke
sana.

2. Uchukue unga baada ya kwisha umuka ukate madonge madonge

3. Weka chuma juu ya moto mdogo wa maka. Kisha uchukue donge
moja ulisukume na uliweke kwa upole ndani ya chuma. Ikiwa unahisi
kuwa unga unaweza kuganda juu ya chuma chako, unaweza kupaka
samli kidogo juu yake. Uufunike kwa mkungu uuchome moto juu na
chini. Baada ya muda mfupi unagalie ukiona umeshatutumka na
umekuwa wa rangi ya manjano utoe uchome mwingine. Endelea hivihivi
mpaka umalize mikate yote.





MKATE WA NYAMA (MSANIF)



Unga kilo moja 1

Nyama3/4

Vitunguu kilo 1

Samli3/4 kilo

Nazi 1

Thomu kiasi

Tangwizi mbichi kiasi

Pilipili manga kiasi

Limau

Chumvi

Hamira kiasi.



1. Saga nyama uikoshe. Kata vitunguu vidogovidogo kama vya sambusa.
Menya thomu uitwange pamoja na tangawizi mbichi na pilpilimanga.
Changanya nyama na vitunguu pamoja na viungo ulivyovitwga utie ndimu na
ukamulie limau. Kisha uipike mpaka ikauke maji iwe kavu, halafu iipue
uitandaze ipowe.

2. Kuna nazi uchuje tui zito. Chunga unga uvuruge kwa tui na chumvi na
hamira halafu uuweke uwache uumuke. Unga usiwe mzito sana.

3. Teleka chuma utie samli kisha teka ung kwa vidole vyako utie juu ya
chuma utandaze duara kiasi cha kitumbua. Halafu chukua kijiko uteke nyama
uitie juu ya ule unga ueenee mote. Teka unga mwengine ufunike ile nyama
yote kisha uchukue kisu uusogeze katikati ya chuma ili uive vizuri. Uuwache
uchemkie juu ya samli na huku ukiugeuzageuza upate kuiva vizuri pindua
upande wa pili uchome kama mwanzo mpaka uive. Unaweza kuchoma
mikate miwili au mitatu kwa wakati mmoja. Choma mikate yote mpaka unga
na nyama umalizike.



MKATE WA NYAMA(MTABAK)



Nyama * kg

Vitunguu maji * kg

Samli * kg

Unga * kg

Mayai 4

Pilpili manga

Bizarinzima

Tangawizi mbichi

V.thomu

B.powder * tsp

Limau

Chumvi.

Njia:

1. Osha nyama iliyokwisha sagwa uichuje maji yote. Vitunguu uvioshe
ubikate vidogovidogo kama vya sambusa. Menya vitunguu thomu usage
pamoja na tangawizi mbichi. Twanga pilipili manga pamoja na bizari
nzima.

2. Changanya nyama na vitunguu pamoja na viungo vyote ulivyovisaga
na kuvitwanga, tia chumvi na limau. Ipike nyama pamoja na vyote
mpaka ikauke, ipua uitandaze ipoe.

3. Chunga unga uufikiche kwa samli iliyoyeyushwa utie baking powder
ukande kwa maji yaliyotiwa chumvi kidogo mpaka ilainike. Ukate unga
madonge mawili. Tia unga mkavu juu ya kibao kusukumia, usukume uendee
kibao chote. Vunja yai moja ulitie kati kati ya unga uliosukuma ulitandaze.
Chukua nyama uitie juu ya lile yai na uitandaze ikae pembe nne, kiasi cha
inchi 6 kila upande. Vunja yai la pili juu ya nyama na baadae ufunike kwa ule
unga uliosalia pembeni kama bahasha ya pembe nne. Fanya mkate wapili
kwa vitu vilivyosalia kama ya kwanza. (kwa sababu vipimo tulivyotoa ni vya
mikate miwili)

4. Teleka chuma juu ya moto utie samli. Ikipata moto tia mkate uuchome
kwa utaratibu. Hautaki moto mkali ukishaiva upande wa kwanza geuza
upande wa pili na ukiiva utoe uchome wa pili hivyo hivyo.







MCHUZI WA NYAMA NA DENGU

Nyama 1kg

Dengu * kg

Vitunguu maji * kg

Nyanya * kg

Samli * kg

Thomu

Zabibu nyeusi kiasi

Bizari nzima kiasi

Iliki

Mdalasini

Limau

Chumvi



Njia:

1. Kata nyama, Osha dengu tia maji na chumvi upike pamoja mpaka
viive.

2. Kata vitunguu, menya thomu usage. Saga nyanya na viungo
vilivyosalia.

3. Teleka sufuria utie samli, ikichemka tia vitunguu uvikaange mpaka vipige
wekundu. Tia nyanya ukaange pamoja na nyama na dengu. Tia maji kidogo
limao na chumvi. Aacha ichemke kidogo. Ukiona kila kitu sawa ipua.



KUKU WA MAHSHAI AU KUKU WA KUJAZA



Kuku 1 mkubwa

Mchele * kg

Samli * kg

Vitunguu maji * kg

Thomu kiasi

Bizari nzima kiasi

Hiliki kiasi

Zabibu kiasi

Chumvi kiasi



Njia:

1. Bila ya kumkata, mchemshe kuku kwa maji na chumvi. Kata
vitunguu, saga thom na viungo vyote uvitie vichemke pamoja akaukie
(bakiza viungo kidogo).

2. Tia Samli katika sufuria utie vitunguu kidogo pamoja na viungo
ulivyovisaga uvikaange. Chemsha mchele kisha uuchuje, utoe maji
yote kisha baadae uutie katika ile sufuria yenye viungo ukoroge pamoja
mpaka ukauke. Fukua kidogo utie zabibu kisha upalie moto kama wali
wa pilau. Kishakauka wali upakue uujaze katika tumbo la kuku na
umshikize kwa uzi mwembamba (yaani umshone) ili ule wali usitoke.
Ikisha mtie kwenye sahani.



BOKOBOKO



Ngano nzima kilo 1 (ikobolewe na isafishwe)

Nyama au kuku 1kg

Samli kidogo,

Chumvi



Njia:

1. Chemsha ngano na nyama upike mpaka viwive viwe laini sana
(usichagnanyishe tina chumvi tu Funika upalie moto.

2. Utakapokauka funua uanze kulisonga bokoboko. Lisonge mpaka
lishikane sawa sawa halafu liipue.

3. Chukua samli uichemshe pamoja na hiliki kisha kila unapo pakua
utakuwa unalilazalaza na kulitengeneza kwa samli. Wengine hupenda
kutengeneza kishimo kati yake na kukijaza samli ya moto. Watu wengine
hupenda kulila tupu. Na wengine hula kwa sukari au kwa mchuzi wake
ambapo hutengenezwa mahsusi.



MCHUZI WA BOKOBOKO



Tende au zabibu 1kg

Samli 1/4 kg

Vitunguu maji kiasi

Thomu

Giligilani

Bizari nzima

Siki

Hiliki

Sukari kiasi.





Njia:

1. Ziroweke zabibu ndani ya maji kisha uzifikiche mpaka zilainike
(usizikamue ukayatoa mashimbi yake). Kama ni tende, zitowe kokwa
uikande na kuzifuruga kwa maji. Mwenye vitunguu menya thomu uvisage
pamoja na viungo vyote.

2. Teleka sufuria utie samli, ikichemka tia vitunguu uvikaange.
Vikianza kupiga wekundu tia viungo vyote, ukaange, kisha tia zabibu au
tende na sukari na siki. Ikiwa maji uliyoroweka tende ni kidogo, ongeza
mengine kidogo acha ichemke kisha ipua.



KASHATA ZA MAYAI



Mayai 15

Samli 1* kg

Sukari 1* kg

Hiliki kiasi

Arki kiasi



Njia:

1. Menya hiliki uzitwange. Vunja mayai yote uyapige kidogo kisha
uyapime, yakiwa yametokea vikombe 15 vya kahawa basi vilevile pima
sukari vikombe 15 vya kahawa na Samli vikombe 15, pima Samli na
sukari kiasi kile kile cha mayai. Sasa changanya mayai, sukari, samli,
arki na hiliki ukoroge mpaka vichanganyike sawasawa.

2. Teleka sufuria upike mchanganyiko huo kwa kuroga bila ya kusita
mpaka ukauke samli ianze kujigida na kutokeza. Hapo tena mimina
katika sinia na utandaze kwa mwiko.

3. Ikianza kupoa chukuwa kisu ukatekate kashata na zikishapoa kabisa
utaweza kuzitoa kwa upole.



KASHATA ZA NJUGU



Njugu nyasa 1kg

Sukari

Hiliki kiasi



Njia:

1. Zikaange njugu uziipue na kuzitoa maganda yote ziwe nyeupe, kisha
uzitwange ziwe unga laini.

2. Chukuwa Sukari changanya na maji kidogo upike mpaka iwe shira nzito.
Twanga hiliki utie, sasa chukuwa unga wa njugu umimine katika shira.
Korogakoroga kwa mwiko mpaka shira ikauke. Kisha mimina haraka katika
sinia iliyopakwa samli kidogo na utandaze. Baadae chukuwa kisu ukate kate
kashata zikisha kupoa zitoe.



KABABU YA NYAMA



Nyama iliyosagwa 1kg

Vitunguu maji *

Samli * kg

Thom kiasi

Tangawizi mbichi

Pilipili manga

Kotmiri fungu 1

Limau 1

Chumvi

Mkate wa boflo 1mdogo

Mayai 4



Njia:

1. Osha nyama katika chujio ivuje maji yote.

2. Roweka mkate wa boflo katika maji katakata vitunguu vidogovidogo,
twanga v. thom na tangawizi na pililimanga.

3. Chukuwa nyama changanya na boflo na vitunguu pamoja na viungo
ulivyovisaga. Tia chumvi, Limau na katia majani ya kotmiri juu yake.
Changanya mpaka vishikane barabara vitu vyote hivyo. Vunja mayai yapige.
Kisha teleka karai itie Samli yote. Chukuwa nyama ifinyange donge kama
ndimu ichovye katika mayai, kisha choma katika karai. Endelea kuchoma
hivyo hivyo mpaka nyama yote imalizike.



UJI WA MAZIWA NA ZABIBU



Unga wa ngano 1/4kg

Zabibu * kg

Sukari * kg

Maziwa pakt 1

Hiliki

Aarki



Njia:

1. Osha zabibu uziroweke katika maji. Menya hiliki uzitwange. Roweka
unga katika maji.

2. Teleka sufuria utie maji kidogo. Yakianza kuchemka chukuwa ule unga
ulouroweka uumimine katika maji, uwe unakoroga huku unatia sukari.
Chukuwa zabibu uzifikiche na kuzikamua, uyachuje maji yote na yatoke
mashimbi yote. Mimina maji ya zabibu katika uji ukoroge. Mwisho tia
maziwa, hiliki na arki. Acha ichemke kwa muda mdogo na huku unakoroga,
halafu uuipue.



FALUDA



Faluda gram 100

Sukari 1/4 kg

Hiliki

Maziwa pakti 1

Aarki kiasi



Njia:

1. Chukuwa majani ya faluda uyatie kwenye maji uteleke juu ya moto
uyechemshe na huku unakoroga koroga mpaka yayayuke. Twanga hiliki utie
pamoja na sukari, arki na maziwa. Acha ichemke na huku unakoroga baadae
ipua utie katika vibakuli ili ipoe igande.





FARNE

Unga wa mchele * kg, (uwe laini sana)

Suakri * kg

Maziwa pakti 1

Hiliki

Aarki

Njia:

1. Uroweke unga katika maji na baadae uchuje kwa kitambaa chepesi.
Menya hiliki uzitwange.

2. Telekea sufuria utie maji kidogo. Yakichemka chukuwa unga uliochuja
kwa kitambaa umimine katika maji ya moto na huku unakoroga. Ukoroge
mpaka uwive vizuri. Halafu ti asukari na huku unakoroga. Mwisho mimina
maziwa na hiliki. Koroga mpaka uchanganyike na uive vizuri bila kuungua.
Usitumie moto mkali sana.

3. Baadae ipua utie katika vijibakuli au visahani vya shimo. Ukisha
poa utaona umeganda mfano wa faluda.







BIRIANI YA SAMAKI



Mchele 1kg

Samaki 1kg

Vitunguu maji 1kg

Samli kiasi

Thomu

Mmdalasini

Hiliki

Ndimu

Nyanya

Chumvi kiasi

Njia:

1. Mkatekate samaki umtie chumvi ndimu umkaange. Menya vitunguu
uvikate. Saga nyanya. Thomu na viungo vyote vilivyosalia. (bakisha
mdalasini nzima kidogo)

2. Teleka sufuria utie samli, ikichemka tia vitunguu uvikaange,
vikianza wekundu tia nyanya na viungo kidogo. Acha vikaange kwa
muda mdogo halafu tia vipande vyote vya samaki, chumvi na ndimu,
pamoja na maji kidogo. Acha ichemke kwa muda mdogo ibaki na rojo
rojo epua.

3. Chukuwa sufuria nyengine uitie maji na chumvi. Yakichemka osha mchele
utie. Acha utokote. Angali kiini wali. Ukiona umewiva umimine uyachuje
maji yote. Teleka tena sufuria pamoja na vile viungo ulivyovisaga. Vyote
vikaange kidogo halafu umimine wali wote ukorogekoroge ili upate
kuchanganyika na viungo. Halafu uweke vizuri upalie moto. Ukishakauka
utaupakuwa. Kuupakuwa kwake utatia wali sahani, baadae ndio utatia
samaki pamoja na rojo rojo zake kwa juu.



NYAMA YA KUIKIZA



Nyama iliyosagwa 1kg

Vitunguu * kg

Nyanya * kg, Samli * kg

Thomu

Bizari nzima

Tangawizi mbichi

Limau

Mayai 6

Chumvi

Mbatata * kg



Njia:

1. Osha nyama iweke katika chujio ivuje maji yote

2. Kata vitunguu. Menya mbatata ukate nyembamba. Saga nyanya,
thomu na viungo vyote vilivyosalia.

3. Teleka sufuria utie samli, ikichemka tia vitunguu uvikaange mpaka vipige
wekundu. Tia nyanya pamoja na mbatata na viungo vyote
vilivyosalia.baadae tia nyama ukaange. Tia chumvi, limau na maji kidogo.
Acha ichemke mpaka ikauke. Kisha ipua. Tafuta legeni la kiasi umimine
nyama yote uiweke vizuri kama mkate. Halafu vunja yai moja baada ya
jengine uyapange vizuri juu ya nyama bila kuharibu viini ukishayatia mayai
yote funika kwa mkunguu palia moto juu yake. Lakini usiwe moto mkali.
Moto mdogo ili usiunguze viini.



TAMBI ZA KUKAANGA



Tambi kavu kilo 1

Sukari * kg

Samli * kg

Hiliki kiasi

Vanila kiasi

Zabibu (zioshe uziloweke kidogo kwenye maji ya moto)



Njia:

1. Zichukuwe tambi uzivunjevunje kwenye sinia au ungo.

2. Teleka sufuria juu ya moto utie samli, ikichemka tia tambi zote uwe
unazikaanga mpaka zipige wekundu. Tia sukari, hiliki au arki pamoja na maji
ya moto. Acha zichemke mpaka uone kiini cha tambi kisiwe laini sana na
maji yote yakauke.

3. Ziipue uache zipoe. Baadae zimimine sahanini. Chukua zabibu
upambie juu yake.



VILEJA



Unga wa mchele 1kg

Sukari * kg

Mayai 6

Hiliki

Arki

Samli * kg



Njia:

1. Uchunge wa mchele kwa chungio lenye tundu ndogo ndogo sana.
Uanike ukauke uwe mkavu sana. Twanga sukari iwe laini uichunge.
Menya hiliki uzitwange.

2. Changanya unga. Sukari, Samli iliyoyeyushwa na arki uwe
unakandakanda kwa kutia mayi kidogo kidogo mpaka ufanyike donge. Kata
madonge madonge uwe unayaweka juu ya kibao na unayatandaza
tararibu,halafu tafuta kibao chenye nakshi ukikandamize juu yake. Kisha
katakata vileja vidogo vidogo kwa namna upendayo, ikiwa vya duara au
kama kashata au vyovyote vile. Fanya hivyo mpaka umalize unga wote.

3. Chukuwa sinia uipake samli, kisha uchome kwa oven juu na chini
kwa moto mdogo mdogo mpaka viwive.



KUKU WA KUCHOMA



Kuku 1 mkubwa

Thomu kiasi

Tangawizi mbichi

Pilipili manga

Ndimu, Chumvi kiasi.



Njia:

1. Mkate kuku vipande na umdugulie chumvi na ndimu. Twanga thomu,
tangawizi na pilipili manga umsugulie. Kisha mweke ili alegee.

2. Washa moto wa makaa kisha uweke uma uwe unamchoma kama vile
unavyochoma mishkaki.

3. Kadhalika kuku wa kukaanga ni hivi hivi isipokuwa badala ya
kuchoma unamkaanga katika mafuta.



KUKU WA KUPAKA



Kuku mkubwa 1

Nazi nzuri 2

Nyanya kubwa 2

Vitunguu kiasi

Limau

Chumvi kiasi

Thomu kiasi

Hiliki kiasi

Njia:

1.Mteleke kuku ndani ya sufuria yenye nafasi bila kumkata, mtie chumvi,
limau na maji kidogo umpike mpaka akauke na aive.



2. Menya vitunguu uvisage, menya thom na hiliki na usage pamoja,
menya nyanya uzisage.

3. Kuna nazi uchuje tuwi zito kisha uvitie vitu vyote ulivyovisaga ndani
ya tui. Lipike na huku unalikorogakoroga mpaka liwe zito na lishikane.

4. Mchukue kuku umtumbukize ndani ya tui uwe una mgeuza mpaka tui
likauke lianze kutoa mafuta.

5. Toa moto wote ubakize vuguvugu. Kisha mfunike umpalie makaa
kidogo. Baada ya muda mfupi muepue.



MCHUZI WA KABABU



Viamba upishi

Nyama iliyosagwa kilo1

Vitunguu nusu kilo

Mbatata

Samli

Nyanya

Bizari nzima

Tangawizi mbichi kiasi

Mdalasini

Hiliki

Majani ya kotmiri

Limau

Chumvi

Njia:

1. Kosha nyama uiweke katika kumto la nazi ivuje maji yote.

2. Kata vitunguu, saga nyanya, menya thomu usage; saga na viungo
vyote vilivyosalia, ila majani ya kotmiri yaoshe uyachambue.

3. Chukua nyama pamoja na nusu ya viungo ulivyovisaga uchanganye.
Tia chumvi pamoja na limau ufinyange madonge madonge kama
kababu. Teleka sufuria juu ya moto utie maji kiasi, chukua zile kababu
uzitie ndani ya maji (lakini hakikisha maji yamechemka) Acha kababu
zichemke ndani ya maji mpaka zishikane bara bara halafu ziipue
uyachuje maji yote. Ziache katika chujio lakini maji usiyamwage.



4. Teleka sufuria utie samli, ikichemka tia vitunguu uvikaange. Vikianza
kuwa vyekundu tia nyanya ukaange kisha tia viungo vyote. Pamoja na
kotmiri, kata mbatata nyembamba uvitie ukaangie pamoja. Tia kababu
ukaange kidogo kidogo kwa utaratibu baadae utie yale maji uliyochemshia
kababu. Tia chumvi pamoja na limau. Acha ichemke. Mbatata ziwive. Ukiona
kila kitu sawa ipua.



SAMAKI WA MAYAI



Samaki nguru 1kg

Vitunguu 1kg

Nyanya 1kg

Samli * kg

Mayai 6

Thomu kiasi

Pilipilimanga

Ndimu

Bizari nzima

Chumvi.

Njia:

1. Mkatekate samaki umtie chumvi, pilipili na ndimu ukaange kisha
mtoe umuweke.

2. Kata vitunguu saga nyanya, thomu na viungo vyote vilivyosagwa.

3. Teleka sufuria utie samli, ikichemka tia vitunguu pamoja uvikaange
mpaka vipige wekundu. Tia nyanya thomu pamoja na viungo vyote vya
samaki uvitie, kisha tia ndimu na maji kidogo kisha onja ukiona kila kitu
sawa vunja mayai moja baada jengine uwe unayaweka juu ya samaki kwa
mpango mzuri bila kuharibu viini vyake. Funika kwa mkungu upalie moto
mdogo mdogo juu yake ili mayai yapate kuiva.

4. Angalia ukiona tayari ipua upakue kwa upole bila kuharibu mpango
wa mayai.



WALI WA ASUMINI



Mchele 1kg

Kuku 1 mkubwa

Vitunguu maji 2kg

Mayai 8

Samli 1kg

Thomu gram 200

Tangawizi mbichi 50gm

Mdalasini 50gm

Hiliki 50gm

Bizari nzima

Siki

Mtindi

Nyanya

Zabibu nyeusi.



Njia:

1. Mkate kuku na umchemshe kwa chumvi na maji mpaka aive, kisha
muipue.

2. Menya vitunguu uvioshe uvikate na uvigawe sehemu 2. sehemu1 uiweke,
sehemu ya pili vikaange mpaka viwe vyekundu kama vya biriani. Kisha
vichuje uitoe samli yote, vitie katika sinia uvitandaze ili vipoe kwa kupata
upepo.

3. Chukuwa mdalasini, Hiliki na bizari utwange pamoja,Kisha uchunge
unge laini.Saga thomu na tangawizi mbichi.Saga nyanya

4. Teleka maji yakichemka tia mchele. Ukiiva utoe uuchuje yatoke maji
yote

5. Teleka sufuria tia samli ie ile iliyokaangiwa vutunguu halfu utie vile
vutunguu vulivyosalia uvkaange. Vikianza kuiva tia viungo ulivyovitwanga
na kuvisaga. (bakisha vitunguu na viungo kidogo). Tia vipande vya kuku,
Mtindi, siki na supu ya kuku iliyosalia katika sufuria. Acha ichemke nyama
pamoja na vitu vyote mpaka ibaki rojo rojo.

6. Teleka tena sufuria tia samli kidogo utie na vile vitunguu
ulivyovisaga uvikaange. Tia mdalasini mzima.kanga pamoja tia na ule
wali ukorogekoroge ili uchanganyike na viungo. Kisha ufunike upalie
moto.

7. Chemsha mayai yote uyamenye.

8. Wali ukishakuka utaupakuwa lakini lazima itabidi utumie kombe au
sahani kubwa itayoweza kuingia wali pamoja na vitu vyote. Kuupakua kwake
kwanza utatia nusu ya wali katika hiyo sahani, baadae utatia masalo pamoja
na nyama yote. Na mayai kisha utayafunika masalo kwa wali uliosalia.
Mwisho utachukuwa vile vitunguu ulivyovikaanga utavitandaza ili vipoe
utavimwaga juu ya wali kwani ni kwa sababu ya hivi vitunguu ndio maana
ukaitwa wali wa asumini. Ukipenda utapambia chembe za zabibu juu yake
zabibu hizo ziloweke kwanza ili zivimbe.



WALI WA BIRIANI



Mchele 1kg

Nyama 1kg

Samli * kg

Mbatata * kg

Vitunguu maji 1kg

Thomu 150gram

Tangawizi mbichi 150gram

Hiliki 50gram

Mdalasini 100gram

Mtindi painti 1

Siki kiasi

Chumvi

Zafarani



Njia:

1. Menya vitunguu naji uvionshe uvikate. Teleka sufuria utie samli.
Ikichemka tia vitunguu uvikaange bila kuvivuruga mpaka viwe vekundu.
Vichuje uitoe samli halafu vitandaze katika sinia.

2. Twanga mdalasini na hiliki mpaka iwe laini kama unga. Menya thomu
uitwange pamoja na tangawizi mbichi.

3. Kata nyama vipande vikubwa kisha tia chumvi na vitu ulivyovisaga
(yaani tangawizi mbichi na thomu) vile vile tia unga wa mdalasini na
hiliki pamoja na mtindi maji. Pika mpaka karibu kuiva kabisa ndipo utie
mbatata. Ukiona mbatata zimeshaiva tia siki usiache ikakauka kabisa.
Bakiza rojo rojo. Tia maji katika sufuria na chumvi yakichemka tia
mchele. Acha utoke angalia kiini cha wali umeshawiva uchuje.

4. Angalia sufuria ya nyama na rojo zake zisiwe zimekauka kabisa,
lazima ziwe na maji kidogo. Chukuwa vile vitunguu ulivyovikaanga
vikipoa vinyunyize juu ya masalo yote usikoroge halafu uite mchele
uliochuja nyunyiza maji ya zafarani juu ya wali halafu unyunyize samli
ile uliyochuja kutoka kwenye vitunguu ulivyovikaanga vienee juu wali
wote. Kisha funika upalie makaa.

5. Wali ukishakuwa tayari utaupakuwa lakini unapotaka kuupakua
lazima kwanza uutowe wali wote mweupe uutie katika chombo kingine,
halafu uyakoroge masalo yachanganyike sawa sawa ndio uyatie juu ya
wali katika kila sahani.



MKATE WA CHILA



Mchele 1kg

Sukari * kg

Nazi 3

Hiliki

Hamira

Samli

Njia:

1. Twanga mchele uwe unga laini, kuna nazi uchuje na kutenga tui zito
mbali na tui jepesi mbali. Twanga hiliki iwe laini.

2. Changanya unga wa mchele, sukari, hiliki na hamira, kisha ufinyange
donge kwa maji ya nazi. Chukuwa hilo donge la unga ulitie kwenye kinu
uliponde mpaka lishikane na lilainike barabara. Litoe ulitie katika bakuli na
ulivuruge kwa kutia tui zito na huku unakoroga kwa upawa mpaka uone unga
umekuwa mwepesi kama uji, ila usiwe mwepesi sana. Tui lililobakia liweke.

3. Chukuwa tui lilosalia ulichanganye na sukari kidogo na hiliki ulipike
na huku unalikorogakoroga mpaka liwe zito zito kisha liipue uliweke.

4. Unga ukishaumuka. Teleka chuma uchukuwe samli kidogo kwa kumbi la
nazi usugulie juu ya chuma halafu teka unga kwa upawa uutie juu ya chuma
ila usiutandaze uuwache utawanyike wenyewe chukuwa mkungu ulio safi
ufunike, baada ya muda mfupi funua utazame ukiona ushakauka utoe mkate
uuweke sahanini.



MKATE WA KUMIMINA



Mchele 1kg

Nazi 3

Mayai 3 ute tu

Suakri * kg

Hiliki

Hamira



Njia:

1. Twanga mchele uwe unga laini. Kuna nazi uchuje tui zito. Twanga
hiliki iwe laini.

2. Pima kila kikombe 1 cha mchele sawa na nusu kikombe cha tui saga
mpaka iwe laini. Tia ute wa yai, sukari , hiliki, hamira.

3. Uwache uumuke ukiwa tayari tia legeni mafuta umimine
mchanganyiko wako na uchome kwenye oven juu na chini.



MKATE WA MAYAI



Mayai 6

Sukari vikombe 3 vya kahawa

Unga wa ngano vikombe 3 vya kahawa

Hiliki

Samli kidogo

Zabibu kiasi

Arki kidogo

B.powder * kijiko cha chai



Njia:

1. Changanya unga mkavu na b.powder.

2. Chukuwa bakuli lenye nafasi na utie sukari. Menya hiliki uzitwange
kisha zichanganye na sukari na utie arki uipendayo. Vunja mayai yote
utie. Chukua mchapo wa kupigia mayai uyapige mpaka yajae kiasi cha
kutosha.

3. Chukua unga uwe unautia na huku unakoroga mpaka umalize wote.

4. Chukua sufuria uipake samli iliyoganda pembezoni mote. Kisha mimina
mchanganyiko wote ufunike. Upike mkate kwenye oven uvivishe juu na chini
angalia moto usiwe mkali sana utaungua mkate ukianza kupiga wekundu
chukua kijiti uchome mpaka ndani ukiona kimetoka kikavu jua kuwa mkate
umeshaiva. Uipue uache upoe baadae utoe kwa upole uweke kwenye sahani.
Chukuwa zabibu tia ndani ya maji ya moto ili zipate kulegea. Baadae
ziipange juu ya mkate. Au unaweza kutia juu ya mkate angali uko juu ya
moto lakini hakikisha kuwa mkate umeshaanza kupiga wekundu ndio uzitie.



VIKATE VYA ZAFARANI



Mchele 1kg

Unga wa ngano * kg

Samli * kg

Sukari * kg

Maziwa painti 1

Mayai 6

Hamira kiasi

Zafarani (iroweke kwa maji ya moto kwenye kikombe cha kahawa)

Njia:

1. Twanga mchele uchunge unga laini. Twanga hiliki. Changanya unga wa
mchele na w ngano. Sukari na hiliki na arki. Tia samli iliyoyeyushwa
ufikiche. Tia hamira na maji ya zafarani na uvunje yai moja na huku
unakanda mpaka yanamalizike mayai yote. Kisha tia maziwa uchanganye
mpaka uwe mwepesi kiasi. Inatakiwa uwe mzito kidogo kuliko wa vitumbua.

2. Teleka kijungu kidogo rashia samli kwa kutumia kumbi la nazi. Kisha
teka unga utie na ufunike. Wacha uive kwa mudamdogo, kisha geuza
bila kutia samli nyengine. Baadae urejeshe tena upande wa mwanzo.
Ukiona umeshakuwa na rangi nyekundu ya kupendeza utoe. Inabidi
uichome mikate hii kwa moto mdogo mdogo sana.



VIKATE VYA JOYA



Mchele 1kg

Sukari * kg

Nazi 3

Hamira kiasi

Zafarani iroweke katika maji moto



Njia:

1. Twanga mchele uchunge unga laini sana. Kuna nazi uchuje tui zito
mbali na jepesi mbali.

2. Changanya unga na sukari uufinyange donge kwa tui jepesi.

3. Kosha kinu kiwe safi sana, utie hilo donge na uliponde kama unavyoponda
unga wa mkate wa kumimina. Utoe ulitie katika chombo utie tui,hamira,
hiliki na ukoroge uwe mwepesi. Ila usiwe mwepesi sana. Uwache uumuke.

4. Teleka maji katika sufuri kubwa halafu uweke kitu chenye tundu
tundu mfano wa waya. Chukuwa vijibakuli vidogo vidogo vilivyopakwa
tui umimine unga ndan yake uvipange vibakuli hivyo juu ya ule waya
wenye matundu, na ufunike na mkungu, acha maji yachemke kwa muda
si chini ya dakika 20. baadae angalia ukiona vimeshaiva vitoe uvitie
sahanini utie dole za safarani juu ya vikate.



MCHUZI WA KIMA





Nyama iliyosagwa kilo moja

Vitunguu * kilo

Nyanya * kilo

Samli * kilo

Thomu kiasi

Bizari nzima kiasi

Hiliki kiasi

Mdalasini kiasi

Chumvi kiasi

Tangawizi kiasi



NJIA:

1. Osha nyama utie katika chujio au kunguto ivuje maji.

2. Kata vitunguu,nyanya,menya mbatata uzikate nyembamba. Menya
thomu usage saga na vuingo vyote vilivyosalia.

3. Teleka sufuria utie samli,ikichemka tia vitunguu ukaange.
Vikanzankupiga wekundu tia nyanya na mbatata, Kaanga kidogo.
Baadaye tia viungo vyote pamoja na limau na chuvi. Acha ichemke
mpaka karibu na kukauka. Onga ukiona sawa ipua









MCHUZI WA MAINI



Maini kilo1

Vitunguu * kilo

Nyanya * kilo

Samli * kilo

Thomu kiasi

Bizar

Bizari nzima kiasi

Pilipili manga kiasi

Tangawizi mbichi kiasi chumvi kiasi.

NJIA:

1. Yakate maini uyaoshe.Menya vitunguu uvisage. Menya thomu usage
pamoja na viunngo vyote vilivyosalia.

2. Yachangavye maini pamoja na vitu vyote hivyo utie na chumvi na
samli, uyateleke. Pika mpaka yakauke maji yote ibake rojo rojo na
samli. Onja, ukiona kila kitu sawa ipua.



SAMBUSA ZA MAFUTA



Nyama iliyosagwa * kilo

Vitunguu * kilo

Unga wa ngano * kilo

Thomu kiasi

Tangawizi mbichi kiasi

Limau kiasi

Unga wa mchele kia

Samli kilo1.



NJIA:

1. Osha nyama utie katika chujio ivuje maji, Kata vitunguu vidogo
vidogo.saga thomu pamoja na viungo vyote. Changanya nyama na
vitunguu pamoja na viungo vyote utie chumvi, limau uipike mpaka
ikauke maji yote. Kisha itandaze ili ipoe.

2. Kanda unga kama wa mkate wa kusukuma, ila huu uwe mgumu kidogo,
halafuukate madonge chukua kibao kipana utie unga wa ngano au wa mchele
halafu uchukue donge moja la unga uanze kusukuma kaki za sambusa.
Sukuma sana mpaka unga uenee kwenye kibao chote, uwe mwembamba
kama karatasi. Kisha chukuwa kisu uukate kwa mstari, kila mstari uwe na
upana wa inchi moja na nusu. Baadae teka nyama kwa kijiko uitie mwanzo
wa kila mstari, halafu ukunje kama sambusa. Endelea kufanya hivyo mpaka
unga na nyama imalizike.

3. Teleka karai juu ya moto utie samli, kabla samli haijaanza kuchemka zitie
unazikaanga kwa moto mdogo mdogo mpaka ziwive, ziwe za rangi manjano.



KATLESI ZA SAMAKI

Mbatata 1kg

Samaki * kg

Samli * kg

Limau

Pilipili manga

Tangawizi mbichi

Majani ya kotmiri fungu 1

Mayai 4

Unga wa tosi kiasi.



Njia:

1. Menya mbatata halafu zichemshe uziponde

2. Mwoshe samaki umtie chumvi na ndimu na ukatie itunguu kidogo.
Kisha umpike awive na akauke maji yote.

3. Saga vitunguu vilivyosalia pamoja na thomu na viungo vyote isipokuwa
majani ya kotmiri, ambayo utayaosha na kuyachambua.

4. Mtoe miba samaki umvuruge pamoja na mbatata majani ya kotmiri
pamoja na viungo vyote ulivyokwisha kuvisaga. Ukande pamoja mpaka
vichanganyike viwe donge laini kisha finyanga katles ndogo ndogo
zenye umbo zuri.

5. Teleka chuma utie mafuta. Yakichemka chukua katles uzigaragarize
kwenye unga wa tosi na uchovye katika mayai na mwishoe uchome
kwenye chuma zikiiva upande mmoja geuza upande wa pili.



SAMBUSA ZA BWANA (Meat Roll)



Nyama ilosagwa * kg

Vitunguu * kg

Mayai 3

Unga wa ngano 1 kg

Siagi * kg

Thomu

Pililimanga

Tangawizi mbichi

Limau

Chumvi



Njia:

1. Osha nyama, kata vitunguu kama vya sambusa, saga thomu pmaoja
na viungo vyote changanya nyama pamoja na vitunguu na viungo vyote
utie chumvi na ukamulie ndimu, kisha uvipike mpaka vikauke.

2. Chunga unga, chemsha siagi kisha ufikiche pamoja. Vunja mayai uyapige
utie na chumvi kidogo halafu ukandie unga. Unaweza kutia maji ya moto
kidogo ili unga ushikane na ulainike.

3. Kata unga vidonge vidogo vidogo usukume duara ndogo ndogo.
Chukua ile nyama uliokwisha ipika uite kwa upande mmoja na upande
wa pili ukunjie juu yake baadae shikanisha unga chini na wa juu kwa
kundamiza pembezoni mote kwa uma ili unapochoma moto ufike mpaka
ndani.



4. Ukisha maliza kusukuma sambusa zote. Ziweke kwenye sinia iliyopakwa
samli ukishazipanga tena mayai kwa kijiko upake juu ya sambusa zote.
Kisha zichome kwa moto mdogo mdogo juu na chini angalia ukiona
zimeshapiga wekundu zitoe uzitie sahanini.



KACHORI



Mbatata 1kg

Samli * kg

Pilipili

Unga wadengu * kg

Chumvi

Bizari ya simba 2

Ndimu 2

Rai kidogo.



Njia:

1. Menya mbatata, zichemshe halafu ziponde ziwe laini

2. Teleka franpen tia mafuta kidogo yakichemka kanga bizari, rai na pili
pili.

3. Halafu changaya na mbatata ulizoziponda pamoja na ndimu

4. Chota mbatata ufanye madonge

5. Chunga unga wa dengu uponde kwa maji

6. Teleka karai na utie mafuta yakichemka chukuwa madonge
uyachovye unga na uanze kuchoma mpaka zipige wekundu zitoe na
kachoti yatari kwa kuliwa.


VITUMBUA



Mchele1kg

Sukari * kg

Nazi kubwa 2

Hiliki

Hamira kiasi

Mafuta

Mayai 4



Njia:

1. Uroweke mchele, kuna nazi uchuje tui zito, menya hiliki uitwange.

2. Chukua kikombe upime kikombe 1 cha tuwi kwa vikombe 2 vya mchele.
Saga mpaka ulainike. Sagia pamoja na ute wa yai na sukari, hiliki na
hamira.

3. Uwache uumuke. Teleka vijungu vidogo tia mafuta yakichemka teka
unga kwa upawa utie kwenye hivyo vijungu na baadae uufunike.
Uwache kwa muda kidogo viive halafu geuza upande wa pili kwa
kutumia kijiti kilichotengenezwa vizuri. Ukiona upande wapili
vishawiva vitoe.





SAMAKI WA KUPAKA



Samaki 1 mkubwa

Nazi 3

Vitunguu * kg

Thomu

Hiliki

Pilipili mbichi

Ndimu nyanya

Chumvi.



Njia:

1. Mwoshe samaki kisha umsagie pilipili na umkamulie ndimu kidogo
kisha umtie katika kijiti au mbano. Mchome kwa moto mdogo awive.

2. Kuna nazi uchuje tui zito zito. Saga vitunguu, nyanya thomu na
hiliki.

3. Teleka tui juu ya moto utie vitunguu pamoja na vitu vyote
ulivyovisaga utie chumvi na ndimu. Lipike tui pamoja na vitu vyote kwa
kulikoroga bila kusita mpaka likauke lianze kutoa mafuta.

4. Mchukue samaki uwe unampaka tui kidogokidogo na huku
unamchoma mpaka tui limuingie sawa sawa.

5. Mtoe samaki katika kijiti au mbano umuweke katika kombe lenye
nafasi kisha uchukue tui lote lililosalia ulipake juu ya samaki.



SAMAKI WA ROJO



Samaki 1mkubwa

Vitunguu 1kg

Nyanya 1kg

Samli * kg

Pilipili manga

Thomu

Ndimu au ukwaju, Bizari nzima, chumvi.



Njia:

1. Mwoshe samaki (usimkate) umtie pili pili, chumvi na ndimu

2. Kata vitunguu, saga thomu, nyanya pamoja na viungo vyote
vilivyosalia.

3. Teleka chuma utie samli ikichemka mtie samaki umkaange vizuri
mpaka aive. Mtoe umtie katika kombe au sahani kubwa ya shimo

4. Teleka sufuria utie samli ikichemka tia vitunguu uvikaange mpaka
vipige wekundu. Tia nyanya na viungo vyote. Tia chumvi, ndimu na
maji kidogo. Wacha ichemke mpaka ikauke. Chukuwa rojo yote
umimine juu ya samaki lakini kwa utaratibu umfunikie wote kwa rojo.



WALI WA PILAU



Mchele 1kg

Nyama 1kg

Samli * kg

Vitunguu maji * kg

Thomu 100gram

Tangawizi mbichi 100 gram

Mdalasini 50g

Hiliki

Bizari nzima

Pilipili manga

Chumvi

Zabibu 100 gram.



Njia:

1. Teleka nyama utie chumvi na maji uipike mpaka iwive. Baadae ipua
uiweke (ubakishe supu itakayotosha kuweza kuivisha mchele).

2. Menya vitunguu uvikate. Twanga thomu, hiliki na tangawizi pamoja na
bizari nzima. Osha vijiti vya mdalasini pamoja na chembe za pili pili manga
uziweke. Osha zabibu uziweke. Menya mbatata uziweke.

3. Teleka sufuria tia samli, ikichemka tia vitunguu uvikaange tia thom
na tangawizi uliyosaga tia vipande vyote vya nyama bila supu. Tia
mbatata na viungo vyote ulivyosaga na kuviosha isipokuwa zabibu
kanga kwa muda mfupi baadae tia supu yote ikianza kuchemka tia
mchele. Onja chumvi. Angalia kiini cha mchele. Ukiona wali umeiva na
kukauka, fukua kati utie zabibu zote na baadae funika upalie moto.



WALI WA CHOOKO



Mchele 1kg

Chooko * kg

Samli kiasi

Nazi 2 nzuri

Thomu

Vitunguu maji kiasi

Hiliki kiasi

Mdalasini kiasi

Chumvi

Karafuu chembe 2 au 3



Njia:

1. Osha mchele pamoja na chooko uweke pembeni.

2. Kuna nazi uchuje tui kama la wali wa nazi uliweke

3. Menya vitunguu maji uvioshe uviweke. Menya vitunguu thomu
uvitwange pamoja na bizari na hiliki. Osha vijiti vya mdalasini na
chembe za karafuu uziweke.

4. Teleka sufuria utie samli, ikichemka tia vitunguu uvikaange baadae tia
viungo vyote ulivyotwanga utie na chembe za karafuu pamoja na vijiti vya
mdalasini. Kisha tia tui la nazi likianza kufumba tia mchele pamoja na
chooko zake utie na chumvi acha utokote mpaka wali ukauke.

5. Ukisha kauka funika upalie moto.



MAANDAZI YA KIPEMBA



Unga 1kg

Sukari * kg

Nazi 2

Hamira

Samli kidogo

Arki

Hiliki

Mayai 3



Njia:

1. Kuna nazi uchuje tui zito. Menya hiliki uitwange

2. Changanya unga, sukari, samli, hiliki, arki na hamira uukande kwa tui la
nazi mpaka uwe laini sana. Ukate unga madonge madonge halafu uusokote.
Tafuta legeni lenye nafasi ulipake samli. Uchukue ule unga uliokwisha
sikota uuweke juu ya legeni kwa nakshi uipendayo. Kisha uuwache uumuke.

3. Unga ukishaumuka usiutoe. Chukua sinia lingine ufunike juu yake na
uyachome maandazi kwa kutia moto mdogo juu na chini.

4. Angalia ukiona maandazi yameshaiva kwa kupiga wekundu yatoe
uyaweke sahanini.



MKATE WA CHANDARUA



Unga * kg

Samli * kg

Chumvi kiasi



Njia:

1. Koroga unga uwe mwepesi, kuliko wa mkate wa maji, na utie
chumvi.

2. Teleka chuma ukipake samli kwa kutumia kumbi. Chovya vidole vyako
katika unga umichie michi juu ya chuma na pembezoni. Acha ukauke kisha
uutoe kwa kisu taratibu bila kuugeuza utaona uwazi kama wa chandarua.



MKATE WA UFUTA



Unga wa ngano 1kg

Nazi 1

Samli * kg

Ufuta kiasi

Hamira

Chumvi.



Njia:

1. Kuna nazi uchuje tui zito.

2. Chunga unga uuvuruge kwenye tui, hamira na chumvi mpaka
ulainike. Usiwe mzito sana kisha uuwache uumuke.

3. Unga ukishaumuka, washa moto na makaa uteleke chuma kilichokoshwa
vizuri. Ikisha pata moto kinyinyize maji ya chumvi. Kata donge la unga
uliweke kwenye chuma litandaze kwa vidole mpaka liwe duara. Chukua ufuta
kidogo kwa vidole unyunyize kwenye unga.

4. Baada muda mfupi geuza chuma ili uso wa mkate upate moto. Mkate
ukibadilika rangi na kuwa mwekundu ubandue kwa kutumia kisu.
Uweke kwenye sahani unyinyize samli iliyoyeyushwa. Hapo mkate wa
ufuta uko tayari kwa kuliwa. Endelea kuchoma mkate mpaka unga
umalizike.







MKATE WA KIAJEMI WA KUKU

Kuku 1 mkubwa

Samli 1 kilo

Unga wa ngano * kilo

Vitunguu maji * kilo

Mayai 8

Limau kiasi

Thomu kiasi

Hiliki Kiasi

Bizari nzima

Chumvi

Zafarani kiasi

Baking powder kiasi.

Njia:

1. Mkate kuku vipande vipande mchemshe kwa maji. Limau, chumvi na
bizari mpaka akauke maji yote na aive.

2. Teleka sufuria mkaange kuku mpaka awe mwekundu kisha umtoe.
Tia vitunguu uvikaange mpaka viwe vyekundu. Saga thom. Hiliki na
bizar nzima utie. Roweka zafarani utie maji yake. Itoe nyama ya kuku
mifupa bila ya kuifuruga halafu itie.

3. Fikicha unga na samli na maji ya moto ukande mpaka uwe laini tia
na baking powder ukandie pamoja. Ukate unga madonge 2 uyasukume
kiasi ya legeni ulilonalo. Lipake samli legeni baadae utie unga
uliosukuma sehemu 1. vunja mayai 4 juu y aunga. Kisha tia vitu vyote.
Tia mayai yaliobakia juu yake yote bila ya kuyapiga. Halafu funika
sehemu ya pili ya unga juu yake uliosukuma umfunike kuku wot na
ushikamane unga wa chini na juu kwa kuusokota sokota pembezoni
kote. Mimina samli iliyochemshwa juu yake kwa kunyunyiza kila
upande na baadae uchome kwa kutumia moto mdogo mdogo juu na
chini mpaka uuive kwa wekundu bila ya kuungua.

4. Ukisha wiva utoe taratibu bila kuuvuruga uutie sahanini.



FILLING

Tungule * kg

Nyama ya kusaga * kg

Jibini 50 gm

Tangawizi

Thomu

Pilipilimanga

Pilipili mbichi

Chumvi

Pilipili boga 2

Vitunguu maji 3.



Njia:

Saga tungule na viungo vyote kwenye blender pasha moto mafuta mimina
tungule na viungo vyote pika mpaka maji yakauke tia kotmiri wacha upoe.
Pika nyama pamoja na viungo kanda unga kwa siagi na maji uwache
uumuke. Baadae ukate madonge 3-4 sukuma kama chapatti lakini iwe kidogo
mnene upike sehemu zote kwa muda wa dakika 5-10 Ondoa na mimina rojo
la tungule nyunyiza nyama. Pamoja na slice za vitunguu tungule na pili pili
boga nyunyiza jimbini oka katika oven 200C mpaka ziwive.







POTATO PIE



Mbatata 400gm

Maji ya ndimu 2

Mayai 4

Tangawizi

Thomu

P.manga

Mdalasini

Vitunguu maji 2

Nyama * kg

Njia:

Osha mbatata chemsha menya na uziponde. Ongeza viungo kwenye nyama
isipokuwa vitunguu maji. Ipike nyama mpaka iive iwache ipoe ongea
vitunguu. Zigawe mbatata ulizoziponda mafungu 2, weka sehemu ya kwanza
trey iliyopakwa mafuta mimina nyama yote itandaze vizuri mimina mbatata
zilizobaki zitandaze vizuri. Mimina mayai yaliyopigwa pigwa juu yake oka
kwenye oven 180C. mpaka iive andaa.



MOUSAKA

Nyama * kg ya kusaga

Mbatatta * kg

Mabilingani 4

Mafuta * kg

Chumvi

Tungule 4

Nyanya ya kopo

Thomu

Tangawizi

P.manga

Uzile

Mdalasini.



Njia:

Kata mabilingani Slices na kuugawa weka upande. Menya mbatata na ukate
vipange kama vya mabilingani kaanga ziwe vyekundu kaanga vitunguu
tungule tia viungo vyote nyama pika kwa muda mfupi ipua. Panga nusu ya
mabilingani kwenye sufuria au treay iliyopakwa mafuta juu yake weka
nyama tena weka mabilingani. Mwisho panga mbatata juu kabisa oka mpaka
iwe nyekundu. Ipua andaa katika hiyo hiyo sufuria.



MEAT CAKE

Njia:

Kausha nyama na viungo vyote vilivyosagwa koroga, teleka katika moto
mdogo mdogo mpaka ikauke epua. Wacha ipoe, piga mayai 3 mimina katika
bati lililopakwa samli, piga mayai 2 changanya na nyama iliyokolea viungo.
Piga tena mayai 3 nyunyiza juu ya nyama choma mpaka iwive.



COCONUT & GROUND NUT QUEENS CAKE



Siagi * kg

Njugu 1kg

Kaanga vunja vunja

Unga 1 kopo B.powder

Nazi 1 ikaange

Mayai 12

Zabibu kiasi Arki

Sukari * kg.



Njia:

Tindia siagi na sukari mpaka iwe laini ongeza mayai, unga na B.powder
mimina nazi na njugu nyengine ubakishe. Paka siagi vibati vyako ti
amchanganyiko kwenye vibati nyunyiza njugu oka mpaka ziwive.





VIKAIMATI



Unga vikombe 2

Maji 1* cup

Hamira 2tsp

Suakri kikombe 1

Arki

Zafarani



Njia:



Chukua unga * kikombe unapiga na hamira na maji * kikombe mpaka uwe
ung'ara na unajivuta sana, uwache uumuke sana upande juu baadae tia unga
(* cup) unatia na maji yalibakia unaupiga tena kiasi sio sana baadae uwache
uumke lakini usiumke sana vinakuwa vibaya.



SHIRA:

Maji 1* cup

Sukari 1 cup

Zafarani & rose essense.

Chemsha maji na sukari mpaka iive iwe nzito kidogo



NANGATAI



Unga laini kopo 2

Sukari kopo 1

Unga wa semolina kopo 1

Mayai 2

Essense

Iliki

Zafarani kidogo

Baking powder 2 tsp

Samli 1kg



Njia:

Saga siagi na sukari kama ya keki iwe nyeupe na nyepesi kisha tia mayai
naaessense (arki) uendelee kusaga, unga changanya na b.powdaer na
zafarani na iliki kisha changanya mchanganyiko wako wa siagi na sukari na
mayai na unga wako kidogo kidogo ili uchaganyike tu usiukande, mwisho
kata vidonge vya kiasi na utie dots juu na uvichome kwa temperature 175 on
middle shelf.





GROUND NUTS BISCUITS



Siagi * kg

Mayi 2

Njugu kiasi

Unga kikopo hicho hicho –3

Arki

B.powder

Coffee kiasi

Sukari kikopo hicho hicho-1 kisijae



Njia:

Roweka njugu zako mpaka zirowane zichambue maganda mpaka ziwe
nyeupe, saga sukari na siagi mpaka iwe nyeupe, tia unga na baking power
changanya. Chukua coffee tia na maji iwe nzito ndani ya kikombe, sukuma
unga kama chapatti halafu tia coffee ya maji juu tandaza mpaka uenee tia
njugu zako juu, kunja kama tabaka, weka ndani ya fridge kwa muda wa
dakika 15. Halafu kata nene, choma kwa umma uate nakshi, paka mayai
yako juu na choma kwenye oven.





MEAT BISCUITS



Siagi * kg

Nyama 1kg

Mayai 3

Unga kopo hilo hilo la * kg

Pilipili

Chumvi

Mayai 3

B.powder

Vitunguu maji

Vitunguu thomu

Tangawizi.



Njia:

Changanya unga, B. powder na siagi kama kawaida, Nyama isage na utie
vitu vyote vinavyotiwa katika nyama ya sambusa, sukuma unga wako uwe
mwepesi kiasi, kata maduara kwa kutumia gilasi yawe mawili mawili. Duara
moja weka chini tia nyama kati na la pili funika juu yake gandanisha bana
kwa dutumia numa. Tia nakshi unayoipenda paka mayai na choma katika
oven mpaka iwe light brown.





BISCUIT ZA MAYAI



Siage * kg

Unga kibati hicho hicho-3

Mayai 12

Nyama1kg

B.powder



Njia:

Fanya nyama yako kama ya sambusa, changanya unga b.powder na saigi
uxhanganyike, tia maji baridi ili ufanyike madonge chamsha mayai na
uyakate sles, sukau unga kama chapatti, kata square 2. moja utatia nyama
halafu juu yake utaweka sles ya yai, na square ya pili utafunika juu.
Gandanisha na ubane kwa uma na utie nakshi zake pembeni mwa ile aquare
paka yai juu yake kwa pamba safi halafu choma kwenye oven. Unaweza
kutumia samaki asie na vumba badala ya nyama.





KASHATA ZA NJUGU ZA KUSAGA(2)



Njugu 1kg

Sukari vikopo 4

Arki kidogo

Maziwa mazito yasiyo na sukari

Au Nido kikopo 1

Maji kikombe 1

Njia:

Unazikaanga njugu mpaka zitoke maganda yote halafu unazisaga unateleka
shira mapaka iwe nzito unatia yale maziwa mazito, unatia arki na
unazimimina zile njugu unasonga kama ugari mwisho unamimina kwenye
sinia iliyopakwa mafuta unapigapiga kwa mwiko tena unaziwacha zipowe
unazikata tena unakula!





MKATE WA TAMBI





Tambi za mchele 2 pkts

Shira

Tuwi

Hiliki



Njia

Unachemsha maji mpaka yanachemka sawa sawa unatia tambi na kutowa
usiziwache sana zitavurugika halafu tia kwenye fran pen halafu tia shira
ambayo umeitia na tuwi (yaani umeipika na tuwi pamoja) unatia juu yake
mpaka zifunike zile tambi halafu juu yake funika foil na uchome kwenye oven
mpaka shira ikauke yote





CHALLA BREAD

Unga vikombe 4-5

Mayai 2

Mafuta or samli * kikombe

Hamira 2 t.spoon

Maji 1 * kikombe

Ufuta na yai

Sukari * kikombe

Chumvi 1 tea spoon



Njia

Unachukuwa vitu vyote hivyo unakanda pamoja ispokuwa ufuta unaukanda
mpaka unakandika sawa sawa halafu unauwacha uumke ukisha umka
unasukuma kama nywele halafu unatia kwenye treya unauwacha tena
unaumka halafu unauchoma kwenye oven juu na chini mpaka uwive.





BOKO BOKO YA NGANO



Kuku 1

Chumvi

Ngano zilizopaazwa vibaba 2

Samli vijiko 2



Njia:

Unamkata kuku kama kawaida halafu unamtia chumvi tu, unamteleka
kwenye jiko unamwacha awive na huku unachukuwa ngano unaziroweka kwa
maji ya moto makali kama saa moja nzima kama yule kuku kawiva sawa
sawa unavuruga na mwiko hapo hapo kwenye jiko lakini awe na maji asiwe
mkavu akishavurugika unatia zile ngano na maji yake unawacha ziwive huku
unakoroga na mwiko huuwachii mkoko ikiwa hazijawiva unaongeza maji
mpaka uhakikishe ngano zimewiva na lishakuwa zito unatia samli na
unaipua na boko boko limekwisha.



MKATE WA MCHELE





Mchele ulorowekwa glass 2

Tuwi glass 1

Hiliki

Ute wa yai1

Sukari * glass



Njia

Unachukuwa mchele na tuwi unasaga kwenye blender mpaka unasagika
usiwe na chenga halafu natia ute wa yai, sukari, hiliki, hamira unasaga
pamoja ikisha unamimina kwenye bakuli unauwancha uumke ukisha umuka
unamimina kwenye fran pen na unauwacha tena uumke ukiwa tayari
unauchoma kwenye oven juu na chini



BASHA MELL (MAKARONI)



Makaroni 1pct

Nyama * kg

Nyanya ya kopo 1

Chumvi

All spices

Maziwa vikombe 5

Unga wa ngano 4tbs

Mafuta 4 tsp



Njia:

Unachemsha macaroni mpaka yawive, chemsha nyama yako mpaka iwive
sawa sawa unaichemshia na spices zote, unateleka sufuria unatia mafuta
viko 4 yakishachemka unatia unga unakoroga huachii mkono mpaka uwive
unatia maziwa kidogo kidogo huwachii mkono unatia na chumvi mpaka
ikisha wiva unaipua halafu mimina nusu yake kwenye yale macaroni na
uchanganye, tia legeni yako mafuta na uchukue macaroni nusu mimina
yatandaze halafu juu yake tia ile nyama itandaze mote halafu malizia juu
yake yale macaroni yalosalia tia ule mchanganyiko wa maziwa uliyapika
ambayo yamebaki nusu yake nyinyizi a mote kwenye macaroni na juu yake
nyunzia mdalasini kwa kufanya kama kadhata halafu tia kwenye oven chini
na juu chini dakika 10 na juu dakika 5 halafu itoe tayrai kwa kuliwa unaweka
mezani na legeni yake.



CHOCOLATE MOOSE



Nestle kikopo 1

Dream box 1

Biscuits maria kubwa 1

Chocolate plain 2

Maziwa glass 1 *



Njia:

Tia nestle na dream kwenye mashine ya keki na usage mpaka vichanganyike
sawa sawa unatia maziwa * glass halafu tia chocolate 1 ambayo iliyokuwa
laini usiiweke kwenye friza, (ikiwa ngumu haisagiki) unasaga mpaka vitu
vyote vinachanganyika sawa sawa. Chukua bakuli la kigae liwe flat chini,
chukua biscuits nusu zichovye maziwa halafu zipange kwenye bakuli
hakikisha haibaki nafasi ziba kwa biscuits halafu juu yake mwaga ule
mchanganyiko nusu yake halafu chukua tena zile biscuits zilibaki panga juu
yake na mwisho juu yake malizia ule mchanganyiko. Chukua chocolate yako
ambayo uliweka kwenye friza hakikisha iwe ngumu ipare kwa kidude cha
kupari chips na unjunyize juu yale ule mchanganyiko halafu weka kwenye
friza muda wa 1 hrs na utoe uikate tayari kwa kuliwa.



ICE CREAM YA LOZI



Maziwa mazito kopo 1 (sona)

Nestle kikopo 1 kidogo

Maziwa mepesi vikopo2 vikubwa (raimbow)

Lozi za kusaga kiasi

Arki

Rose



Njia:

Chukuwa vitu vyote hivyo visage kwenye blender unasaaga mpaka
mchanganyiko wote uchanganyike sawa sawa halafu tia kwenye bakuli la
kigae ililokuwa chini flat mimina huo mchanganyiko na utie kwenye friza
mpaka igande tayari kwa kuliwa.



SUPERGETTI YA KUKU



Supergeti 1pct

Kuku 1

Cheese ya kupara

Tomato fresh 4



Njia:

Unapika rosti lako kama kawaida la kuku mkate vipande vidogo vidogo
halafu unatia super get ulizochemsha lakini unachanganya pole pole ili
yasivurugike halafu unamimina kwenye legeni lako juu yake unanyinyiza
cheese uiliyoipara unaweka kwenye oven 15 minute only.



MCHUZI WA ADESI



Adesi * kg

Mbatata 2

Vitunguu maji 2

Carrot 1

Tungule 4 fresh

Pili pili boga 1

Nyanya kopo 1

All spices

Mafuta 3 tsp



Njia:

Unachukua adesi unazichemsha zinawiva halafu unachukuwa sufuria jengine
unakaanga mchuzi wako ukisha kuwa tayari unatia zile adesi unaangalia na
kiasi cha uzito unaotaka halafu unaipua.



FISH FINGER



Samaki (jodari) kiasi vipande 6

Mkate wa boflo uliorowekwa 2 midogo

Mdalasini

Uzile

Pilipili manga

Ndimu1

Unga wa tosi

Mayai



Njia:

Unamshemsha samaki mpaka anawiva halafu unavuruga na mkono halafu
unatia spices zote pamoja na mkate wa boflo unachanganya pamoja
uhakikishe mchanganyiko umekolea. Unafanya vidonge disegn ya kidole
halafu unachovya yai n aunagaragariza kwenye unga wa tosi baadae
unazichoma kwa mafuta mpaka ziwe nyekundu unazitoa.



BUTTER BOLLS

Siagi * kg

Njugu za kusaga

Unga wa ngano 1kg

Sukari * kg

Mayai 2

Jam kiasi

Baking powder 2 spoon

Njia:

Unasaga siagi na suakri mpaka isagike iwe laini unatia mayai unasaga tena
unatia na b.powder unasaga tena halafu unatia unga unachanganya kwa
mkono. Kata madonge na usukume kwenye kibao na ukate desig ya duara
kati tia kidole paka yai juu unyunyize njugu na utie jam halafu choma
kwenye oven juu na chini moto size 150. mpaka vipige wekundu kidogo
unavitoa.



PUDDING



Maziwa 1 litre

Mayai 4

Hiliki

Sukari vijiko 6vikubwa

Arki kidogo



Njia:

Chukua mayai yapasulie kwenye blender changanya na maziwa, sukari, hiliki
na arki halafu viblend weka sufuri ndogo injika sufuria kubwa kwenye moto
weka maji lita3 na yaache yachemke yakianza kutoa mvuke, chukua sufuria
ndogo yenye mchanganyiko wa maziwa itumbukize kwenye sufuria yenye
maji ya moto hakikisha umeifunika vizuri isipitishe mvuke iwache dakika 15
halafu ipua sufuria ndogo iweke pembeni bila kuifunua mpaka ipoe na uitoe.



PIZZA – MEAT

Nyama * kg

Yai 1

Unga wa ngano glass 1 ya bati

Maziwa kikombe 1 cha kahawa ya unga

Hamira

Carrot

Pilipili boga

Tungule

Cheese

Tomato Source + Paste

Samli

Sukari 1tsp

Chumvi



Njia:

Unaukanda unga wako kwa yai, maziwa, samli ,chumvi, sukari, hamira
unaukanda mpaka unakuwa laini sana. Unauwachaa uumuke, chukuwa
nyama uichemshe na spices mpaka inakuwa kavu halfu ikaange na tomato
paste mpaka ikauke ipua. Chukua fran pen pakaza siagi chukuia unga
uliokwisha umuka sukuma kwenye kibao kama chapari uwe sana na fran pen
yao halafu uweke juu ya frean pen pakaza tomato sourse kidogo halafu
mimina nyama yako tia carrot ulizopara kama chps pamoja na P.boga kata
tungule slices panga juu yake na upare cheese utie juu halafu choma kwenye
oven mpaka mkate uwive. Itoe halafu uikate kabisa triangle.



VILILI



Samli 1kg

Sukari 1kg

Unga kiasi

Hiliki



Njia:

Chukua samli na sukari usage mpaka ilainike pamoja na hiliki, tia unga
uchanganye pamoja kiasi cha kufanyia vidonge fanya shape unayotaka na
uchome kwenye oven lakini visiwe vyekundu moto uwe mdogo mdogo.



TUTTY FRUITS



Siagi 1kg

Sukari 1kg

Unga mabati 1 * kg

Mayai 6

B.powder 3tsp

Jam kiasi

Njugu au korosho kiasi

Arki.



Njia:

Saga siagi na sukari mpaka vilainike, halafu tia mayai 4 uanchangya na arki
au hiliki, halafu unachanganya na unga na b.powder. saga njugu au korosho
ziwe vipande vipande, sukuma donge la unga lisiwe nene sana kisha tandaza
jam juu yake nyunyiza njugu au korosho zilisosagwa. Kunja kama
pen-hweels na kata size unayotaka ikisha paka yai juu yake na uchome.



KARA BISCUITS

Siagi 1kg

Unga mabati 2

Mayai 2



Njia:

Siagi unaigawa * kg na unabakisha * unachanganya unga na siagi hiyo ya *
kg mpaka ichanganyike tia maji baridi na fanya madonge hakikisha unga
unakuwa mgumu. Sukuma kama mkate na pakaa siagi kunya sehemu nne na
sukuma tena fanya hivyo hivyo kiasi cha mara 2 au 3, kata size unayotaka,
pakaa mayi juu na choma.



BISCUITS ZA TANGAWIZI



Siagi * kikombe

Sukari kikombe 1

Yai 1

Unga utakisia

Sukari ya kuunguza * kikombe

B. powder 2tsp

Tangawizi 1tsp

Karafuu 1tsp.



Njia:

Saga siagi na sukari tia yai , sukari ya kuunguza na vitu vyote vikavu
vilivyobaki. Changanya pamoja tengeneza duara ndogo ndogo tia kwenye
tray iliyopakwa samli na choma.



ROCK CAKE



Siagi 1kg

Sukari 1kg

B.p 3 tsps

Unga mabati ya 1kg 4

Kungu manga

Mayai 1 dosen

Tangangawizi

Hiliki au arki

Ukitaka njugu au korosho



Njia:

Unasaga siagi na sukari mpaka ilainike iwe nyepesi na nyeupe changanya
unga na viungo vyote na ile sukari uliyoipiga na siagi vunja mayai na
uchanganye na mchanganyiko wako wa kwanza mpaka uwe kiasi,(yamalize
yote) nyofoa vidonge vigogo vidogo na uchome hadi viwe light golden brown.



ROCK BUNS



Unga * lb

Sukari * lb

Siagi 2 oz

Mayai 2

Maziwa kiasi

Zabibu

B.p 2tsp



Njia:

Vuruga siagi, sukari unga na vitu vikavu vyote, tia mayai na maziwa kanda
pamoja. Pakaa samli kwenye sinia, ikisha pondea unga tia kwenye sinia
ikisha fanya madonge choma kwenye oven kwa dakika 15.



ALMOND SLICES



Unga 8 oz

Siagi 4 oz

B.powder 1tsp

Lozi 3 oz

Apricol jam 1tbsp

Yai 1



Njia:

Fikicha siagi na unga uliochanganywa na B.powder. Tia sukari changanya
ute wa yai kanda vizuri sukuma mstari mnene * in na upana uwe 3in price
well choma Finya finya pembe kwa pembe kwa mapambo. Pakaa jam kaati
kati piga ute na sukari na mpaka iwe nzito koroga katika sukari na pakaa juu
ya jam, nyunyiza llozi na choma kwenye mabati yaliyopankwa samli kata
vipande wakati imoto.





DOUGHNUTS (DONAS)



Unga mabati 3

Samli 1kg

Hiliki kiasi

Kungumanga kiasi

B.powder 3tsp

Mayai 1dosen

Sukari



Njia

Fikicha unga na samli na hiliki, kungumanga na B.powder na sukari ya
kusaga mkono mmoja (1) Piga mayai na changanya unga mpaka ufanyike
madonge, sukuma mpaka upate unene unaoutaka halafu kata mkato wa
donas choma kwenye mafuta ya moto kisha ipua na pale pale ugaragaze
katika ile sukari iliyosagwa halafu weka pahala penye upepo vipowe.





PUDDING YA POVU



Sukari * lb

Maziwa 2pints

Mayai 8

Badamu 8

Zabibu kiasi

Pista

Hiliki



Njia

Vunja mayai na uweke ute na viini mbali mbali. Teleka maji yachmke piga
ute mpaka uwe mzito,Tia ndani ya sufuria yenye uffuniko unaobana, na utie
hiyo sufuria ndani ya sufuria ya maji yaliyochemka na ufunike baada ya
muda utizame kama hainati toa tia zabibu na lozi juu yake piga vile viini
pamoja na sukari mpaka iwe nazito tia maziwa na hiliki weka juu ya mota
mdogo mdogo na koroga ikiwa nzito ipua wacha ipoe tia kwenye shani ya
shimo na utie ile pudding ya ute wa mayai juu yake taratibu ili usiharibike
ukipenda tia rangi tatu green, red, yellow na ubakishe nyeupe sehemu moja
yaani zote ziwe sehemu 4



LADU



Unga wa dengu 1lb

Sukari 1 lb

Zafarani kiasi

Samli * lb

Baking powder 1tsp

Rangi ya biriani kiasi

Njia:

Vuruga unga wa dengu kama badia na B.p Teleka samli ndani ya karai tia
unga ndani ya karai. Toa tia ndani ya kumgo halafu mbio mbio tia ndani ya
kinu utwange. Pika sukari nzito tia na kufanya madonge.



BISCUITS ZA VIDOLE





Unga kibaba 1 *

Siagi * kg

Tende * kg

Samli kikombe1

Ufuta kiasi

Mayai 5 moja liwe la kupaka



Njia

Chambua tende teleka samloi ndani ya sufuria ikichemka tia tende na
uisonge iksha iwache ipoe changanya unga na siagi mpaka iwe kama chenga
za mkate. Piga mayai na anza kunyunyiza kidogo kidogo mpaka
unachanganyika ongeza maji ya baridi ili ufanyike madonge, Kata madonge
na uwanze kusukuma donge la kwanza na tende ufanye madonge 2 chukua
donge la tende na uliweke juu ya lile donge la unga ulilolisukuma na
ukukume juu yake hadi donge la tende lisukumike liwe sawa na la unga
baadae unauroll unga wote wa kwenye kibao ikisha unakata vipande kwa
kisu. Piga yai na anza kupaka juu ya vile vipande ulivyovikata ikisha juu
yake nyunyiza ufuta hatimae vichome moto mdogo mdogo.



QUEEN'S CAKE



Siagi1 * oz

Yai1

B.powder 1 * tsp

Sukari 1 * oz

Maziwa 1 * oz

Ganda la limau

Unga 1 * oz

Zabibu kavu 1 tsp

Njia

Saga siagi na sukari kama kawaida piga yai na uwongeze juu yake hadi iwe
laini ule mchanganyiko ongeza ganda la limau, zabibu na uchanganye kidogo
kidogo katika ule mchanganyiko n uwongeze maziwa ukoroge kidogo kidogo
kwa kuifold in paka tray mafuta na nyunyiza unga kidogo kidogo tia
mchanganyiko wako katika kila kishimo tia 1tbsp. Choma katika oven
templ180-150c kwa dakika 10-15



KEKI YA JABALI(ROCK CAKE)



Unga wa ngano

Siagi 2 * oz

Yai 1

Sukari 2 * oz

Hamira 2 tsp

Zabibu kavu 1tb.sp



Njia:

Washa oven 400 F-270 c na paka mafuta legeni na nyunyiza unga kidogo
chaekecha unga hamira na chumvi kwenye bakuli kubwa fikicha siagi na
unga huo hadi mchanganyiko ufanane na chaenga za mkate ongeza sukari na
zabibu na changanya vyema oangeza mayai na maziwa ili ushikamane
mchanganyilo tumia umma na weka mchanganyiko ndani ya legeni vidonge
vifanane na jabali weka ndani ya oven kwa dakika 20.



COCONUT BUNS



Unga wa ngano 4 oz

Hamira 1 tsp

Nazi iliyokunwa 1 oz

Siagi 2oz

Yai1

Maziwa 1 * tb.sp

Chumvi kidogo



Njia:

Chekecha unga hamira na chumvi kwenye bakuli. Ongeza siagi na fikicha na
changanyisha vyema. Ongeza sukari na nazi, Cahanganya vizur vunja yai na
upige pige vizuri na ongeza kwenye mchanganyiko ushikane vizuri,Weka
mchanganyiko kwenye tray yenye shimo lililopakwa mafuta na tia kwenye
oven temp 200c kwa dakika 20.



MELTING MOMENTS



Unga –1kg

Siagi * kg

Mayai 5

Sukari 275 gms

Baking powder 6tsp

Vanilla essense 2tsp

Corn Flakes

Jam

Njia:

Chunga unga wako na uchanganye na baking powder mayai weka viini mbali
na ute mbali. Kisha saga sukari hadi iwe laini halafu saga siagi na sukari
hadi iwe cream yaani kama ya keki, kisha tia vile viini vya mayai endelea
kupiga pamoja mpaka vichanganyike na utie arki ya vanila uchanganye,
mwisho tia unga wako kidogo kidogo uchanganye kwa mkono hadi
uchanganyike uwe donge (lakini usiukande) sasa tia trey yako samli (ipake)
na ufanye vidonge vyako vya duara uvipake ule ute wa yai na uvigaraze juu
ya vile cornfkaes ulizozikata vipande kisha uvipange juu ya trey na ubonyeze
kwa kidole juu yake ili vifanye vishimo viwache viumuke baadae tia tray
yako kwenye oven uviwache viwive visiwe vibichi wala visiwe vyekundu
viwe vyeupe. Viwache vipoe. Mwisho tia jam yako ndani ya vile vishimo au
kama unazo cherries kata vipande utie ktk kila kishimo.



SABAH ALLY SEIF AL RIYAMI TOBBY



EMAIL:

chabby/at/fromzanzibar.com OR
princesschabby/at/hotmail.com

ZANZIBAR – TANZANIA

 

2004-11-06